Shirikisho la Afrika ya Kati
Shirikisho la Afrika ya Kati (liliitwa pia Shirikisho la Rhodesia na Unyasa) lilikuwa dola la kujitawala chini katika mfumo wa ukoloni wa Uingereza uliounganisha nchi za leo za Zambia, Zimbabwe na Malawi zilizoitwa wakati ule Rhodesia ya Kaskazini, Rhodesia ya Kusini na Unyasa (Nyassaland).
Lilipatikana kati ya mwaka 1953 hadi mwisho wa 1963.
Shirikisho lilianzishwa tarehe 1 Agosti 1953 kwa shabaha ya kuunda nchi itakayofuata njia kati ya muundo wa ubaguzi wa rangi ya Afrika Kusini upande mmoja na nchi huru zilizotawaliwa na wanasiasa Waafrika wenye mwelekeo wa Ujamaa. Lilikuwa jaribio la kutunza kipaumbele cha walowezi wenye asili ya Ulaya.
Mwisho ulikaribia baada ya miendo ya kumaliza ukoloni duniani kote na nguvu ya wawakilishi wa Waafrika katika eneo la shirikisho iliongezeka nguvu.
Mwisho wa mwaka 1963 Rhodesia ya Kaskazini ilikuwa taifa jipya la Zambia na Unyasa (Nyassaland) ikawa Malawi.
Rhodesia ya Kusini ilibaki peke yake ikitangaza uhuru wake miaka kadhaa baadaye na baada ya vita vya ukombozi kuwa nchi ya Zimbabwe.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |