Nenda kwa yaliyomo

Wayoruba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kundi la Wayoruba katika picha ya pamoja

Wayoruba (kwa Kiyoruba: Ìran Yorùbá, Ọmọ Odùduwà, Ọmọ Káàárọ̀-oòjíire[1]) ni kabila la Afrika Magharibi ambalo linaishi sehemu za Nigeria, Benin na Togo zinazounda nchi ya Yoruba, lakini pia Ghana.

Wayoruba wanajumuisha takriban watu milioni 45 barani Afrika, wapo laki kadhaa nje ya bara, na wana uwakilishi zaidi miongoni mwa wanachama wa diaspora kutoka Afrika, hasa Brazil na Kuba.

Idadi kubwa ya Wayoruba leo wako ndani ya nchi ya Nigeria, ambapo wanaunda 15.5% ya wakazi wa nchi hiyo, kulingana na makadirio ya CIA[2], na kuwafanya kuwa moja ya makabila makubwa zaidi barani Afrika.

Watu wengi wa Kiyoruba huzungumza lugha ya Kiyoruba, ambayo ni lugha ya Niger-Kongo yenye idadi kubwa zaidi ya wazungumzaji asili[3].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]