Oasisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kupata English band, tazama Oasis (bendi). Kwa matumizi mengine, tazama Oasis (maana)


Ein-Kelt, an Oasis in the Judean Desert, Israel

Katika jiografia, Oasisi au cienega (kusini magharibi mwa Marekani) ni eneo la mimea lililotengwa katika jangwa, kwa kawaida likizunguka chemchemi au kitovu kingine cha maji. Oasisi pia hutoa makazi kwa wanyama na hata binadamu kama eneo ni kubwa vya kutosha.

Maeneo yenye oasisi yamekuwa muhimu kwa biashara na njia za usafiri katika maeneo ya jangwa. Misafara hulazimika kupitia karibu na oasisi ili kujiongezea hazina zao za maji na chakula. Hivyo, kudhibiti kisiasa au kijeshi Oasisi mara nyingi kuna maanisha kudhibiti biashara ya misafara fulani. Kwa mfano, oasisi ya Awjila, Ghadames na Kufra iliyoko katika Libya ya leo, kwa nyakati mbalimbali zimekuwa muhimu kwa biashara za Kaskazini-Kusini na Mashariki-Magharibi katika biashara ya Sahara. Neno Oasisi lilikuja kuingia katika Kiingereza kutoka neno la Kigiriki ὄασις Oasis , lililotoholewa moja kwa moja kutoka neno la Misri wḥ3t au Demotic wḥỉ . Haikutoholewa kutoka kwa Coptic ouaḥe (* / waħe /), kama inavyopendekezwa wakati mwingine; neno la Kigiriki limedhibitishwa karne kadhaa kabla ya Coptic kuwepo kama lugha iliyoandikika[onesha uthibitisho].

Oasisi ya Huacachina katika Ica, Peru


Oasisi hutokana mito iliyo chini ya ardhi au aquifer kama vile artesian aquifer, ambapo maji yanaweza kufikia juu kwa shinikizo la kimaumbile au kwa watu kuchimba visima. Gharika fupi za mara kwa mara hutoa maji chini ya ardhi na kuendeleza oasisi, kama vile Tuat. Miamba na mawe iliyo chini ya ardhi na isiyopenyeza maji inaweza kuyateka maji na kuyahifadhi katika mifuko; au katika sehemu ndefu chini ya ardhi zenye maeneo hafifu au mitaro ya volkeno maji yanaweza kukusanyika na kububujika juu ya ardhi. Matukio yoyote ya maji hutumiwa na ndege wakihama na pia kupitisha mbegu pamoja na mavi yao ambazo hukua kandokando ya maji haya na kutengeneza Oasisi.

Kupanda mimea[hariri | hariri chanzo]

Oasisi katika sehemu ya Sahara ya Libya

Watu wanaoishi katika Oasisi hawana budi kusimamia matumizi ya ardhi na maji kwa makini; mashamba lazima yanyunyiziwe maji ili kukuza mimea kama vile tende, tini, mizaituni na apricoti. Mmea muhimu zaidi katika Oasisi ni mitende ambao hutengeneza safu ya juu. Mitende hii hutoa kivuli kwa miti midogo kama vile ya Peach, ambayo huwa katika safu ya katikati. Kwa kupanda mimea katika tabaka mbalimbali, wakulima hutumia ardhi na maji bora zaidi. Mboga nyingi pia hukuzwa na baadhi ya nafaka, kama vile ngano, shayiri na mtama hukuzwa katika maeneo yenye unyevu zaidi. [1]

Oasisi maarufu[hariri | hariri chanzo]

Afrika[hariri | hariri chanzo]

Amerika[hariri | hariri chanzo]

Fish Springs National Wildlife Refuge, Utah, Marekani.

Asia[hariri | hariri chanzo]

Ein Gedi, Israeli

Australasia[hariri | hariri chanzo]

Ulaya[hariri | hariri chanzo]

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

Makala ya Waandishi[hariri | hariri chanzo]

  • (Kifaransa) Marejeo: Jardins au Desert (Vincent Battesti)

| Battesti (Vincent), Jardins au desert, Evolution des pratiques et savoirs oasiens, Jérid tunisien, Paris, Editions IRD, coll. À travers champs, 2005, 440 p. ISBN 2-7099-1564-2 Open Archives: book in free access / in French

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]