Mwaprikoti
Jump to navigation
Jump to search
Mwaprikoti (Prunus armeniaca) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Mwaprikoti unaochanua
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Mwaprikoti ni mti mdogo wa familia Rosaceae. Matunda yake huitwa maaprikoti. Asili ya mti huu haijulikani, kwa sababu ulipandwa sana kabla ya historia. Sikuhizi hupandwa mahali pengi katika kanda za nusutropiki.
Kwa kawaida, jina la mwaprikoti hutumika kwa spishi P. armeniaca, lakini P. brigantina (mwaprikoti-milima), P. mandshurica (mwaprikoti wa Uchina), P. mume (mwaprikoti wa Japani) na P. sibirica (mwaprikoti wa Siberia) yanahusiana sana na matunda yao pia huitwa aprikoti. Matunda haya hayapatikani katika Afrika.