Nenda kwa yaliyomo

Haile Mariam Desalegne

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Haile Mariam Desalegne

Haile Mariam Desalegne (* 19 Julai 1965 Boloso Sore, Wolayita, Ethiopia) ni mwanasiasa wa nchini Ethiopia. Mwaka 2010 alikuwa waziri wa mambo ya nje na makamu wa waziri mkuu wa Ethiopia. Baada ya kifo cha waziri mkuu Meles Zenawi terehe 20 Agosti 2012 alikuwa waziri mkuu mtendaji.

Haile Mariam ni kiongozi wa kwanza wa kitaifa anayetoka katika kusini ya Ethiopia na pia mkristo wa kiprotestant wa kwanza katika uongozi wa juu.

Haile Mariam alizaliwa mwaka 1965 katika wilaya ya Boloso Sore kwenye kanda la Wolayita lililopo katika kusini ya Ethiopia. Familia yake ni sehemu ya kundi la Wawolayta na wakristo; tofauti na asilimia kubwa ya Wawolayta Haile Mariam anafuata aina ya ukristo wa kipentekoste katika kanisa la Hawariyat (Kanisa la kimitume la Ethiopia)[1]

Baada ya kumaliza shule ya sekondari alihamia Addis Ababa aliposoma uhandisi hadi digrii ya kwanza. Alirudi katika kusini ya nchi akafanya kazi kwenye taasisi ya teknolojia ya maji huko Arba Minch. 1990 alitumwa kwa masomo ya juu kwenda Tampere, Ufini aliposoma hadi digrii ya pili akarudi kama master in sanitation engineering. Akaendelea kufanya kazi ya taasisi ya teknolojia ya maji hadi kuwa mkuu wake. Wakati wa kupanda ngazi katika taasisi alijiunga na chama tawala cha Ethiopia EPRDF.

Mwanasiasa

[hariri | hariri chanzo]

Haile Mariam hakushiriki katika shughuli za mapinduzi yaliyopindua udikteta wa kikomunisti wa Mengistu mwaka 1991 maana wakati ule alikuwa masomoni huko Ufini. Lakini baada ya ya kujiunga na EPRDF aliteuliwa mwaka 2000 kuwa makamu wa rais la jimbo la Mataifa ya Kusini na tangu mwaka 2001 hadi 2006 pia raisi yake.

Mwaka 2005 aliingia katika siasa ya kitaifa kwa njia ya kuchaguliwa mbunge. Wakati uleule alikuwa pia mshauri kwa ofisi ya waziri mkuu Meles Zenawi. 2008 alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kindu la EPRDF katika bunge la Ethiopia.

Zenawi alimfanya makamu wake na waziri wa mambo ya nje mwaka 2010. Baada ya kifo cha Zenawi alikuwa waziri mkuu mtendaji.


  1. Jörg Hausteina* & Terje Østebøb: EPRDF's revolutionary democracy and religious plurality: Islam and Christianity in post-Derg Ethiopia. Journal of Eastern African Studies, Volume 5, Issue 4, 2011 (Special Issue: Ethiopia's revolutionary democracy, 1991–2011), pages 755-772