Nenda kwa yaliyomo

Meles Zenawi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Meles Zenawi

Meles Zenawi (*9 Mei 1955 - 20 Agosti 2012) alikuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia tangu 22 Agosti 1995 hadi kifo chake. Alitangulia kuwa rais wa nchi kati ya 28 Mei 1991 na 22 Agosti 1995. Alifuatwa na makamu wake Haile Mariam Desalegne.

Historia yake

[hariri | hariri chanzo]

Zenawi alikuwa mwanafunzi wa tiba kwenye chuo kikuu cha Addis Ababa wakati wa mapinduzi ya kikomunisti ya Ethiopia ya mwaka 1974. 1975 aliacha masomo akarudi kwake Tigray akajiunga na Harakati ya Ukombozi wa Tigray TPLF iliyopinga serikali mpya. Tangu 1985 aliongoza TPLF. 1989 alikuwa mwenyekiti wa ushirikiano wa TPLF na vikundi vingine vya upinzani kutoka sehemu mbalimbali za Ethiopia.

Baada ya kupinduliwa kwa serikali ya kikomunisti ya Mengistu katika Mei 1991 Zenawi aliteuliwa kuwa Rais.

1995 katiba ilibadilishwa. Cheo cha Waziri Mkuu kilikuwa cheo chenye uzito kuliko rais na Zenawi alihamia katika ofisi ya waziri mkuu.

Elimu na maisha ya binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Meles Zenawi ameshika shahada ya MA ya utawala wa biashara kutoka Uingereza na MSc ya uchumi kutoka Uholanzi.

Amemwoa Azeb Mesfin; wana watoto watatu. Inasemakana Meles anapenda kusoma, kuogelea na tennis.