John Agyekum Kufuor

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
John Kufuor

John Kofi Agyekum Kufuor ( 8 Desemba 1938 mjini Kumasi, Ghana) ni mwanasiasa. Alikuwa rais wa 11 wa Ghana tangu 7 Januari 2001 hadi 7 Januari 2009.

Uchaguzi wake ulikuwa badiliko la kwanza la mkuu wa nchi kufuatana na katiba bila kuingilia kwa jeshi. Alipata asilimia 48,4 za kura katika awamu ya kwanza wa uchaguzi akachaguliwa na 52,45% katika awamu ya pili akimfuata raisi mtangulizi wake Jerry Rawlings.

Kufuor amezaliwa katika kabila la Waashanti na familia ya Wakristo wakatoliki. Baada ya shule alisoma chuo cha Premeph College mjini Kumasi akaendelea kusoma sheria na siasa kwenye chuo kikuu cha Oxford (Uingereza) hadi digrii ya kwanza. 1961 akawa mwanasheria katika Uingereza.

Tangu kurudi Ghana alijiunga na utumishi wa serikali akawa kaimu waziri wa mambo ya nje na mwakilishi wa Ghana kwenye Umoja wa Mataifa na Umoja wa Muungano wa Afrika kati ya 1969 na 1971.

1969 alikuwa kati ya waanzilishaji wa chama cha maendeleo (Progress Party -PP) na 1979 akashiriki katika kuundwa kwa chama cha Popular Front Party (PFP). Hadi mapinduzi ya kijeshi ya 1972 na mapinduzi ya Rawlings ya 1981 alikuwa mbunge na kila safari alikamatwa na kutupwa jela kwa muda.

1996 aligombea urais mara ya kwanza akashindwa na Rawlings. 1998 akatangazwa tena kama mgombea wa chama cha New Patriotic Party akateuliwa pia kuwa kiongozi wa chama. Mwaka 2000 alimshinda makamu wa Rawlings katika kura ya uraisi.

Alimwoa Theresa Mensah na kuzaa watoto 5 naye. Familia yote hushiriki katika kansia katoliki.