Ukimwi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Upungufu wa Kinga Mwilini (kwa kifupi UKIMWI; kifupi cha Kiingereza AIDS) ni ugonjwa unaotokana na virusi inayoitwa HIV au kwa Kiswahili VVU na inayoshambulia mwili kwa kuondoa nguvu zake za kupambana na maradhi.

Ukimwi ni ugonjwa hatari sana katika maisha ya mwanadamu kwa kuwa huweza kusababisha kifo (yaani kupotea kwa uhai wa mwanadamu huyo). Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, kufikia mwaka 2014 ugonjwa huu umeua watu milioni 39, hasa wanaoishi barani Afrika upande wa kusini kwa Sahara. Kwa mwaka 2015 pekee wamefariki watu milioni 1.2 na kati yao watoto wengi.

UKIMWI hadi hivi sasa haina dawa, lakini tunaweza kuuepuka ugonjwa huu kwa kuachana na ngono ambayo huweza kusababisha ugonjwa wa ukimwi, pia tunaweza kujikinga na ugonjwa huo kwa kuepuka kuchangia vifaa au vitu vyenye ncha kali.

Tarehe 1 Desemba kila mwaka ni siku ya UKIMWI duniani.

Virusi ya UKIMWI ikitoka seli.

Maana ya jina[hariri | hariri chanzo]

UKIMWI ni kifupi cha "Upungufu wa Kinga Mwilini"

 • Upungufu maana yake UKIMWI unaharibu uwezo wa mwili kupambana na magonjwa. Si UKIMWI moja kwa moja unaoweza kuua lakini mashambulio ya magonjwa ambayo kwa kawaida yasingekuwa tatizo kubwa.
 • Kinga inahusu mfumo wa kingamwili ambao ni uwezo wa mwili kujitetea dhidi ya ugonjwa.
 • Mwili usio na kinga unapatwa na matatizo mbalimbali kwa sababu mfumo wa kinga umeharibika, na hauwezi kupigana na ugonjwa wowote.

Jina la Kiingereza ni AIDS= Acquired Immuno Deficiency Syndrome.

 • acquired - maana mtu hawezi kuwa na hali hii kiasili, ameipata
 • immuno - hii inataja ya kwamba tatizo linahusu "immune system" yaani mfumo wa kingamwili
 • defiency - inamaanisha ya kwamba kuna kasoro
 • syndrome - ni mkusanyiko wa matatizo ya kiafya; ilhali kingamwili haufanyi kazi tena mgonjwa anaathiriwa na magonjwa mbalimbali na kuonyesha dalili za magonjwa hayo yote.

Mfumo wa kingamwili na virusi za HIV[hariri | hariri chanzo]

Kila mtu huwa na mfumo wa kingamwili ndani yake. Seli za ulinzi zinazunguka mwilini na kutafuta vidubini vya nje vinavyoweza kuleta mvurugo na zinaviharibu. Kati ya seli hizi za ulinzi ni seli nyeupe za damu (lukosaiti) ambazo ni muhimu sana.

Ukimwi unasababishwa na virusi za HIV. Kama virusi zote, HIV inaingia katika mwili kwa kusudi la kuzaa. Virusi haiwezi kuzaa peke yake. Inahitaji seli inapoweza kuingia ndani yake na kutumia mfumo wa seli kwa kunakili DNA yake.

Kwa kawaida virusi zinashambuliwa na mfumo wa kingamwili na kuharibika. Lakini virusi za HIV zina tabia mbili za pekee ambazo zinazifanya za hatari hasa

 • zinafaulu mara nyingi kuepukana na seli za ulinzi mwilini
 • zinaingia hasahasa katika seli nyeupe za damu za aina "seli za T". HIV ikianza kuongezeka katika seli nyeupe ya damu inadhoofisha na hatimaye kuharibu seli hii.

Maana yake virus ya HIV inashambulia moja kwa moja seli ambazo ni sehemu ya kingamwili na zinazohusika kukinga mwili. Kuenea kwa virusi za HIV mwilini kunapunguza idadi ya seli za ulinzi na hivyo kupunguza kiwango cha ulinzimwili.

Baada ya kupungukiwa kwa kingamwili vidubini vingine vinaendelea kufika mwilini lakini sasa vinaenea zaidi kwa sababu seli za ulinzi zimekuwa chache. Kila ambukizo linaendelea kwa muda mrefu zaidi na mwili kwa jumla unateswa kwa muda mrefu zaidi. Kadiri Ukimwi unavyoendelea zaidi vipindi vya magonjwa yanaendelea kuwa virefu zaidi na nguvu za mwili zinapunguapungua. Katika ngazi za mwisho idadi ya maambukizo inazidi uwezo wa mwili wa kupambana nayo na hapo mtu unakaribia kifo.

Watu wangapi wana UKIMWI?[hariri | hariri chanzo]

Idadi ya watu duniani wenye VVU miaka 1979-1995
 A map of the world where most of the land is colored green or yellow except for sub Saharan Africa which is colored red
Asilimia ya watu wenye umri wa miaka 15–49 walioambukizwa nchi kwa nchi (2011).[1]

Mwaka 2015 walau watu wapatao 36,700,000 walikuwa wakiishi na VVU. Watu wengi wenye VVU hawajui kuwa nayo. Kwa sababu hiyo, idadi halisi ya watu wanaoishi na VVU haijulikani.

Wengi kati ya watu wenye VVU huishi katika Afrika. Wengi kati ya watoto ambao hufariki dunia kutokana na UKIMWI pia wanaishi barani Afrika.

Wapi VVU ilianza[hariri | hariri chanzo]

Wanasayansi wengi wanaamini binadamu wa kwanza ambaye alipata VVU (kwa Kiingereza HIV) alikuwa Afrika Magharibi ya Kati. Hii ilitokea mwishoni mwa karne ya 19 au mwanzoni mwa karne ya 20, wakati virusi ya SIV kutoka kwa nyani au sokwe ilikwenda kwa binadamu.

VVU na UKIMWI[hariri | hariri chanzo]

Si kila mtu aliye na VVU ana UKIMWI. Wakati watu wanapata VVU, wanaweza kuwa na afya kwa miaka mpaka akakutwa na aina maalumu ya magonjwa na vipimo vya damu vikionyesha kuwa ina idadi ndogo sana ya seli nyeupe za damu ambazo ndizo zinazopambana na maambukizi.

Kuna maradhi ambayo kwa kawaida ni ishara kwamba mtu ana UKIMWI kwa kuwa watu wenye afya njema hawapati magonjwa haya, kwa sababu mfumo wa kinga mwilini una nguvu ya kutosha ya kupigana na magonjwa hayo. Hivyo kupata ugonjwa wa aina hiyo ni ishara kwamba mfumo wa kinga umeharibika.

Baadhi ya magonjwa hayo ni:

Matibabu[hariri | hariri chanzo]

Kuna dawa za kusaidia watu wenye UKIMWI. Hizi zinaitwa dawa za kurefusha maisha. Dawa za kurefusha maisha haziwezi kutibu UKIMWI. Hii ina maana kwamba haziwezi kufanya virusi vyote kuondoka mwili wa mtu. Lakini zinaweza kuwasaidia watu kupambana na virusi vya UKIMWI kwa mifumo yao ya kinga kufanya kazi vizuri zaidi. Hivyo dawa za kurefusha maisha si tiba kabili kwa virusi ya UKIMWI.

Watu wenye VVU / UKIMWI ambao huchukua dawa za kurefusha maisha wanaweza kuishi muda mrefu, bila kupata maradhi yanayothibitisha UKIMWI.

Lakini baada ya muda mrefu, virusi za HIV zisizouawa na dawa hizo hujifunza jinsi ya kupambana nazo na hivyo zinakuwa sugu kwa dawa hizo.

Wakati mwingine HIV ni sugu kwa dawa moja, lakini dawa nyingine inaweza kutumika. Ili kupunguza uwezekano wa upinzani kutokea, watu wenye UKIMWI huchukua dawa zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Wanaweza kuchukua madawa 2-4 kwa mara moja. Hii wakati mwingine inaitwa cocktail ya UKIMWI. Lakini baada ya muda mrefu, HIV kujifunza kuwa sugu kwa dawa nyingi. Hapo hakuna zaidi ya kuwatibu. Hivyo wanasayansi kuendelea kujaribu kupata dawa mpya ya kupambana na VVU.

Dawa tano muhimu za wenye VVU ni:

 • D4T (stavudine)
 • 3TC (Lamivudine)
 • NVP (nevirapine)
 • AZT (zidovudine)
 • EFZ (efavirenz)

Bila dawa hizo, kwa kawaida mtu mwenye VVU anaweza akaishi miaka 9-11.

Mayatima[hariri | hariri chanzo]

Asilimia ya watu waliokuwa wanaishi na VVU katika Afrika miaka 1999-2001

Watu wengi ambao wanakufa kutokana na UKIMWI, hasa katika Afrika, huacha watoto ambao bado ni hai, na ambao wanaweza wanahitaji msaada na huduma.

Njia za kujikinga na UKIMWI[hariri | hariri chanzo]

Kuna njia nyingi za watu kupambana na janga hilo.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Njia muhimu kwa kuzuia VVU / UKIMWI ni elimu. Watu wanaweza kupata VVU kutokana na ngono na kutokana na damu. Watoto wanaweza pia kupata VVU kutoka kwa mama zao (wakati wa kukua ndani ya akina mama wajawazito na wakati wa kunyonya maziwa ya mama.)

Vitendo vya kijinsia ni njia kuu ya kupata VVU. Kama watu wanatumia kondomu wanapofanya mapenzi, kuna nafasi ndogo zaidi ya kuambukizwa VVU, lakini ukweli kamili ni kwamba hakuna ngono salama kwa hakika.

Mtu anaweza pia kupata VVU kwa kuchangia sindano. Hii ina maana ya kutumia sindano ambayo haijawahi kusafishwa baada ya mtu mwingine kuitumia. Baadhi ya watu ambao kinyume cha sheria huchukua madawa ya kulevya kama heroin na cocaine huchukua dawa hizo kwa sindano. Baadhi ya watu hawa wanachangia sindano moja. Kama mtu mmoja ana virusi ya UKIMWI na anashirikisha sindano yake, anaweza kuambukiza HIV kwa watu wengine.

Kuna baadhi ya watu ambao hawataki watu kujua kuhusu kondomu na sindano safi, au hawataki watu kuwa na kondomu au sindano safi. Hao wanaamini kuwa watu wakijua kuhusu kondomu na kuwa na kondomu watafanya ngono zaidi na hivyo kuzidisha maambukizi. Vilevile wanaamini kuwa watu wakiwa na sindano safi watatumia dawa za kulevya zaidi. Wengi wa hao watu wanadhani hii pia kwa sababu ya dini zao zinazokataza uzinifu na ulevi.

Chanjo dhidi ya HIV[hariri | hariri chanzo]

Njia bora ya kuzuia VVU ni wazo la kuwa na chanjo, lakini hakuna chanjo kwa HIV bado. Wanasayansi wengi wanatafuta chanjo ya VVU ili kuokoa mamilioni ya maisha ya watu.

Utepe mwekundu - ishara ya mapambano dhidi ya UKIMWI

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

 1. AIDSinfo. UNAIDS. Iliwekwa mnamo 4 March 2013.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Rod of Asclepius2.svg Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ukimwi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.