Ukahaba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Picha ya mfano wa kahaba akiwa kazini.

Ukahaba (kutoka ar. قحبه qahabatun = malaya) ni tendo la kufanya ngono nje ya ndoa au uhusiano unaokubalika katika jamii, tena na watu mbalimbali na kwa malipo. Watendaji wanaopokea malipo huitwa kahaba au malaya; washiriki wanaotoa malipo huitwa wateja. Kama ukahaba unaendeshwa katika nyumba maalumu mahali panaitwa danguro.

Jinsi na namna ya ukahaba[hariri | hariri chanzo]

Kimsingi kuna aina mbili za ukahaba.

  1. Malaya anajifanyia kazi na kuamua mwenyewe namna gani. Huyu atapatikana mara nyingi akitembea barabarani, kusubiri kwenye mabaa au kwa kutangaza namba ya simu. Wanajitangaza pia kupitia intaneti na kukutana na wateja mahali mbalimbali.
  2. Malaya wanafanya kazi chini ya usimamizi wa mtu mwingine au watu wengine. Hali yao inaweza kufanana na aina ya ajira wakilipwa kwa kila tendo la ngono kutoka msimamizi anayepokea fedha; au wanatakiwa kutoa malipo kwake kutokana na mapato yao.

Kundi hili lapatikana mara nyingi katika danguro lakini wako pia barabarani katika maeneo maalumu wanapotazamiwa na kuwadi. Katika kundi hili kuna hasa aina ya utumwa wa kingono ambako mabinti na wanawake wanalazimishwa kujiuza kwa wateja.

Sheria kuhusu ukahaba duniani      Ukahaba unaruhusiwa, kuna utaratibu wa kisheria      Ukahaba unaruhusiwa, danguro ni marufuko, hakuna utaratibu wa kisheria      Ukahaba ni marufuku      hakuna habari juu ya nchi hizi

Hali ya kisheria[hariri | hariri chanzo]

Misimamo ya jamii na sheria inatofautiana kati ya nchi na nchi. Hata kama ukahaba unapatikana kote duniani umepigwa marufuku katika nchi nyingi. Lakini mahali pengi penye sheria dhidi ya ukahaba polisi inafunga macho au kutofuatilia biashara hii.

Kati ya misimamo kuhusu ukahaba iko ifuatayo:

  • Ukahaba hutazamiwa kama jinai. Watendaji wanatishiwa kwa adhabu za kisheria kuanzia faini, jela hadi adhabu ya mauti (kama Saudia). Mara nyingi ni hasa makahaba wanaolengwa kwa adhabu hizi, lakini mahali pengine pia wateja. Hata hivyo katika nchi nyingi penye sheria dhidi ya ukahaba polisi inafunga macho au kutofuatilia biashara hii.
  • Ukahaba hutazamiwakama ubaya unaovunja heshima hasa ya wanawake yaani malaya. Malaya huangaliwa kama waathirika wanaostahili kusaidiwa kwa hiyo hawana adhabu. Lakini wote wengine wanaofaidika na ukahaba wanalengwa kwa adhabu: wenye danguro, makuwadi, washiriki katika biashara ya makahaba hadi wateja wenyewe katika nchi kadhaa (mfano: Uswidi)
  • Ukahaba hutazamiwa kama ubaya usioshindikana kwa hiyo serikali imetunga sheria na taratibu kwa lengo la kupakana upatikanaji wa ukahaba. Danguro zinapaswa kuandikishwa serikalini, zinatembelewa na idara ya afya ya umma; malaya wanaruhusiwa katika mitaa maalumu ya miji pekee, wanapaswa kuangaliwa na matibabu mara kwa mara. Vijiji na miji midogo zinaweza kuzuia ukahaba katika maeneo yao.
  • Ukahaba hautazamiwi tena kama jinai wala kosa bali kama chaguo la watu wazima. Kwa hiyo ukahaba huangaliwa kama namna ya biashara kama biashara nyingine; malaya huitwa "wafanyakazi wa ngono" wanatakiwa kulipa kodi na wanalindwa na sheria za kazi (mifano Uholanzi na Ujerumani).
  • Utaratibu maalumu uko katika Uajemi ambako kuna "mutaa" au ndoa ya muda kulingana na mafundisho ya Kishia. Chini ya utaratibu wa mutaa kuna uhusiano uaolingana na ndoa au pia urafiki katika nchi nyingine; lakini mutaa inaruhusu pia mikataba kwa muda mfupi na inadai mapatano juu ya malipo upande wa mwanaume. Kwa hiyo inapatikana pia kama njia ya ukahaba ambao menginevyo ni arufuku nchini Uajemi.


Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
Blank template.svg Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ukahaba kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.