Nenda kwa yaliyomo

Klamidia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Vijududu vinavyosababisha klamidia

Klamidia ni ugonjwa wa kuambukiza ambao husababishwa na bakteria wanaoitwa katika uainishaji wa kisayansi Chlamydia trachomatis.

Ugonjwa huo huwa hauonyeshi dalili za wazi kwa karibia asilimia 75 ya wanawake na asilimia 50 ya wanaume, hivyo maambukizi mengi hushindwa kufahamika mapema. Watu ambao hawajafahamu kuwa wameambukizwa klamidia wanaweza wasitafute tiba na hivyo wakaendelea kufanya ngono, bila ya kujua kuwa wanaeneza ugonjwa.

Wakati dalili zinapoanza kujitokeza wanaume husikia maumivu wakati wa kukojoa au kutokwa usaha au uchafu pamoja na kupata mwasho katika uume. Wanawake wanaweza kutokwa damu nje ya kipindi chao, kukojoa mara kwa mara, maumivu wakati wa kukojoa, kutokwa usaha au majimaji machafu katika uke, mwasho kwenye uke na maumivu chini ya kitovu au sehemu za nyonga.

Kama utaachwa bila kutibiwa katika wanawake, klamidia inaweza kuleta madhara makubwa kwa afya ya binafsi na ya jamii. Klamidia huaribu tishu za uzazi za mwanamke na kusababisha uvimbe katika fupanyonga (pelvic inflammatory disease, PID). PID inaweza kusababisha mauvimu makali sana katika fupanyonga, utasa/ugumba au utata katika ujauzito ambao unaweza kusababisha kifo. Wanawake wenye bakteria hao wana urahisi mkubwa hadi mara tano zaidi wa kuambukizwa Virusi vya UKIMWI.

Watoto waliozaliwa na mama aliyembukizwa klamidia huwa na hatari ya kupata upofu au maambukizi katika mapafu.

Utambuzi

[hariri | hariri chanzo]

Utambuzi wa maambukizi ya klamidia hufanyika kwa kuchunguza fupanyonga na kiwango kidogo cha majimaji kutoka katika uke au uume ambayo huchunguzwa kwa uwepo wa Chlamydia trachomatis. Uchunguzi mpya kama ule wa mkojo ili kufahamu uwepo wa bakteria wa klamidia umekuwa ukitumika pia ili kufanya uchunguzi rahisi zaidi wa watu ambao hawaonyeshi dalili za ugonjwa.

Klamidia inatibika kwa antibiotiki.

Duniani mwaka 2015 wagonjwa walihesabiwa kuwa milioni 61, wengi wakiwa Afrika na Asia Kusini. Kulingana na wakala wa afya wa Marekani Centers for Disease Control and Prevention ndiyo ya kwanza kati ya maradhi ya zinaa yanayoripotiwa zaidi nchini humo: wataalamu wamekadiria kuwa karibia watu milioni tatu huambukizwa klamidia kila mwaka, lakini maambukizi 1,600,000 tu ndiyo ambayo huripotiwa.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Klamidia kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.