Maambukizi nyemelezi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Magonjwa nyemelezi, ambayo unaweza kuyapata baada ya kuambukizwa ugonjwa wa ukimwi, ni kutokwa na jasho wa usiku, kutokwa na vipele mwilini au ukurutu, kuwashwa sehemu za mikononi na miguuni, kuharisha mfululizo zaidi ya mwezi mmoja, kutapika, kutokwa na tezi sehemu za shingoni, kuishiwa nguvu mwilini, kutokwa na mafua, kukosa hamu ya kula, maumivu makali kiunoni au mgongoni na kupelekea kuathiri akili, kupotea kwa kumbukumbu akilini, kuambatana pamoja na kifua kikuu, kuumwa na tumbo, kupungua uzito zaidi ya asilimia kumi.

Hizi dalili hutokea baada ya miezi mitatu mbele, na si kila dalili uipatayo kati ya hizi una ugonjwa wa ukimwi, ila ni vyema kwenda hospitalini kucheki mwili wako sababu dalili hizi hutokea na kupotea sababu vijidudu vya ugonjwa wa ukimwi huwa vinapambana na kinga mwilini, baada ya kinga kushindwa magonjwa nyemelezi ya hapo juu yanaaza kujitokeza upya; ni vyema kwenda kupima hospitalini na kupata ushauri wa daktari na jambo tu la kukumbushia ugonjwa huu hauna dawa wala chanjo, ni janga kubwa kwa taifa zima na gharama zake ni kubwa mno.

Kwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huu ni vyema kuanza dozi au kutumia dozi ipasavyo kwa muda mwafaka sababu ugonjwa huu ukiacha tu kutumia dozi wadudu hawa wanajizalisha upya tena kwa kasi na dozi hiyo haiponeshi bali inawafanya wadudu wa HIV walewe ili wasiendelee kujizalisha na kuupa mwili nguvu.

Rod of Asclepius2.svg Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maambukizi nyemelezi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.