Kuvu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Fungi)
Kuvu (Fungi)
Kuvu kwenye matunda yanayooza
Kuvu kwenye matunda yanayooza
Uainishaji wa kisayansi
Domeni: Eukaryota
Himaya: Fungi
Ngazi za chini

Faila, nusufaila

Blastocladiomycota
Chytridiomycota
Glomeromycota
Microsporidia
Neocallimastigomycota

John Carroll Dikarya (inc. Deuteromycota)

Ascomycota
Pezizomycotina
Saccharomycotina
Taphrinomycotina
Basidiomycota
Agaricomycotina
Pucciniomycotina
Ustilaginomycotina

Nusufaila Incertae sedis

Entomophthoromycotina
Kickxellomycotina
Mucoromycotina
Zoopagomycotina

Kuvu (jina la kisayansi kutoka Kilatini: Fungi) ni kiumbehai ambacho si mmea wala mnyama. Uainishaji wa kisayansi unavipanga katika himaya ya pekee ndani ya Eukaryota. Kati ya kuvu kuna viumbe vikubwa kama uyoga na pia vidubini yaani vidogo vyenye seli moja tu kama hamira au maungano ya seli kama koga.

Utaalamu wa kuvu unaitwa mikolojia.

Kuvu zinatokea kwa namna mbalimbali

Tofauti kati ya kuvu, mimea na wanyama[hariri | hariri chanzo]

Zamani vilihesabiwa kati ya mimea lakini lishe yao ni tofauti. Mimea inategeneza chakula chao au mata ogania inayohitaji kwa njia ya uanisinuru yaani kwa njia ina lishe autotropia. Kuvu inatumia mata ogania iliyopo tayari sawa na wanyama hivyo lishe yake ni heterotropia. Kuvu hutumia mabaki ya miili ya mimea na wanyama wengine na kuyatumia kama chakula chake.

Tofauti na wanyama wengi kuvu haitembei na muundo wa seli zake ni tofauti; seli za wanyama huwa na ngozi ya nje bali seli za mimea na kuvu huwa na ukuta wa seli. Tena tofauti na mimea kuta za seli ni za chitini si selulosi jinsi ilivyo kwa mimea.

Hadi sasa kuna spishi 70,000 zinazojulikana na kuna makadirio ya kwamba jumla inaweza kupita milioni 1.

Kuvu mbalimbali
Seli za hamira chini ya hadubini

Maumbile[hariri | hariri chanzo]

Kuvu hutokea kwa maumbo mawili:

  • seli moja-moja kama hamira. Zinazaa hasa wa njia ya kujigawa.
  • miseli ambayo ni kama nyavu inayojengwa na nyuzi za kungunyanzi; hizi ni seli ndefu umbo la neli zinazoshikana na kuwa uzi ndefu. Inaonekana katika nyuzi nyeupe zianzoonekana katika chakula kinachoanza kuoza maana yake kuoza kwa mkate nis awa na fungu kukua ndani yake. Zinazaa zaidi kwa njia ya spora zinazofanana na mbegu za mimea.

Kuvu ni jumla ya kungunyanzi zote na jumla hii huitwa miseli. Miseli ya aina hii inaweza kuenea mbali sana ikikua ndani ya ardhi kwa mfano msituni inayopata lishe kutoka kwa majani, matawi na mashina yaliyoanguka chini. Kama kiumbehai miseli haina umbo maalumu lakini kuna mifano ya miseli moja iliyoenea hektari zaidi ya 30 na kushi miaka 1,000 angalau.

Kwa aina kadhaa miseli inajenga sehemu za pekee zinazotoka kama uyoga. Uyoga si kuvu mwenyewe bali kitu kama tunda lake. Unajengwa na nyuzi nyingi za kungunyanzi na kuwa mahali pa kukuza spora ambavyo ni kama mbegu za kuvu.

Ekolojia[hariri | hariri chanzo]

Kuvu ni muhimu katika ekolojia ya viumbehai huwa na athira kubwa.

Zikitumia mata ogania ya viumbe vingine kazi yao ni kuvunja miili ya mimea na wanyama. Ni kuvu pekee zinazoweza kuvunja mata ya ubao na kuipasua katika kemikali zake. Pamoja na bakteria na wanyama wadogo hutengeneza ardhi yenye rutba.

Kuvu zinashirikiana na mimea. Takriban asilimia 80-90 za mimea yote zina kuvu kwenye mizizi yao. Hapa inaishi pamoja katika simbiosi au mtoshelezano. Maana yake nyuzi za kungunyanzi za kuvu inaingia ndani ya ardhi kushinda mizizi midogo ya mmea. Hivyo kuvu inasaidia kupata madini na mata ya lishe kutoka ardhi kuchinda mmea mwenyewe. Usaidizi huu unaonekana hsasa kwa mazao kwenye ardhi isiyo na rutba nzuri sana; kuvu huboresha lishe ya mimea. Kwa upande mwingine kuvu inavuta hidrati kabonia kutoka mzizi zinazojengwa na mmea kwa njia ya usanisinuru.

Uyoga ya champignon hulimwa kibiashara kama chakula ni tunda la miseli

Kuvu na kibinadamu[hariri | hariri chanzo]

Kuvu zina athira pia kwa binadamu.

Kuvu katika chakula[hariri | hariri chanzo]

Vinywaji kama pombe, bia au divai vinategemea kuvu za hamira.

Kinyunga cha mkate kinachachuka vilevile kutokana na hamira.

Chakula na sumu[hariri | hariri chanzo]

Kuvu hutoa pia madawa na sumu. Chakula kinachooza mara nyingu huwa na miseli ambayo ni sumu kwa wanadamu. Hata sehemu za uyoga ni sumu kali. Kinyume chake aina nyingine za uyoga ni chakula bora kwa sababu ni chanzo cha protini nzuri.

Chanzo cha madawa[hariri | hariri chanzo]

Kuvu mbalimbali zimetumiwa kwa kutoa madawa ya kutibu magonjwa. Dawa la penicillin linapatikana kutoka kwa kuvu pamoja madawa mengine ya kiuavija (antibiotic). Zinatoa pia madawa ya kuzuia mbu.

Kuvu kati ya vidole (mamunyumunyu)

Magonjwa[hariri | hariri chanzo]

Kuvu zinatokea pia kwenye mwili kama magonjwa. Kuvu inaanza kukua kwenye sehemu za ngozi kama mwili unakosa kinga (tiba). Inatokea hasa mguuni na kujulikana kwa jina la nyungunyungu au mamunyumunyu; kama mguu hausafishwi mara kwa mara inaonekana kama vidonda kati ya vidole.

Ugonjwa mgumu zaidi ni kukua kwa kuvu kwenye ngozi za utumbo. Wakinamama huathiriwa mara nyingi na kuvu ndani ya uke.

Uharibifu wa majengo[hariri | hariri chanzo]

Kuvu pia humea kwenye kuta, dari na mapaa ya majengo hasa ya ghorofa[1]. Ukuta unapolowa maji na hewa kuwa na unyevu wa juu kuvu hukua na kuenea si tu kwa kuta bali pia kwa fenicha. Kuvu inapoenea huharibu rangi ya kuta na huacha kuta zikiwa zimechakaa.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kuvu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.