Nenda kwa yaliyomo

Ngono zembe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ngono salama)
Tangazo la Marekani dhidi ya uzinifu wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Ngono zembe maana yake ni tendo la ndoa lililofanywa au linalofanywa kwa uzembe, yaani bila kujali matokeo yake, hasa maambukizi ya maradhi ya zinaa, na kwa namna ya pekee Ukimwi.

Katika jamii, na hata mbele ya Mungu ni kosa kusababisha madhara bila sababu, hasa kama ni kuendeleza maradhi yanayomtesa binadamu, yanahitaji tiba ya gharama kubwa, na hatimaye yanaweza kuleta kifo cha wengi.

Baadhi ya watumiaji wanataka kumaanisha kufanya ngono bila kondomu, kama kwamba kutumia mpira huo kungetosha kuleta usalama kwa wahusika. Kumbe siyo, kwa sababu kondomu inapunguza uwezekano wa maambukizi (katika nchi zilizoendelea kwa asilimia 70-85), lakini haiwezi kuyazuia kabisa[1][2].

Kinyume chake, inawezekana kufanya tendo la ndoa bila kondomu wala uzembe kwa sababu linafanywa na watu waaminifu wasio na ugonjwa wa namna hiyo. Hivyo wako salama tu.

Tafiti kadhaa bara Afrika zimeonyesha kwamba tohara inaweza kupunguza maambukizi ya wanaume kwa asilimia 60[3], lakini wengine wanapinga.[4][5]

Kwa vyovyote Kusini kwa Sahara mabadiliko ya tabia na matumizi ya kondomu yameonekana kufanikiwa zaidi na bila gharama ya tohara.[6]

  1. "The American Heritage Dictionary of the English Language, Fourth Edition, Houghton Mifflin Company, 2009, Accessed 23/09/09". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-11-29. Iliwekwa mnamo 2014-08-11.
  2. Vittinghoff E, Douglas J, Judson F, McKirnan D, MacQueen K, Buchbinder SP. (1999). Per-contact risk of human immunodeficiency virus transmission between male sexual partners. Am J Epidemiol. 150(3):306-11. PMID 10430236
  3. "WHO agrees HIV circumcision plan", BBC World News, BBC, 2007-03-03. Retrieved on 2008-07-12. 
  4. Circumcision and HIV
  5. "Circumcision and AIDS". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-07-23. Iliwekwa mnamo 2014-08-11.
  6. Mcallister RG, Travis JW, Bollinger D, Rutiser C, Sundar V (Fall 2008). "The cost to circumcise Africa". International Journal of Men's Health. 7 (3). Men's Studies Press: 307–316. doi:10.3149/jmh.0703.307. ISSN 1532-6306.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: