Abacavir
Muundo wa kikemikali wa abacavir | |
Jina la Utaratibu la (IUPAC) | |
{(1S,4R)-4-[2-amino-6-(cyclopropylamino)-9H-purin-9-yl]cyclopent-2-en-1-yl}methanol | |
Data ya kikliniki | |
Majina ya kibiashara | Ziagen, others[1] |
AHFS/Drugs.com | Monograph |
MedlinePlus | a699012 |
Taarifa za leseni | EMA:[[[:Kigezo:EMA-EPAR]] Link], US Daily Med:link |
Kategoria ya ujauzito | B3(AU) C(US) |
Hali ya kisheria | POM (UK) ℞-only (US) |
Njia mbalimbali za matumizi | Kwa mdomo (kiowevu au vidonge) |
Data ya utendakazi | |
Uingiaji katika mzunguko wa mwili | 83% |
Kimetaboliki | Ini |
Nusu uhai | 1.54 ± 0.63 h |
Utoaji wa uchafu | Figo (1.2% abacavir, 30% 5'-metaboliti ya asidi ya karboksi, 36% 5'-metaboliti ya glukuronidi, 15% Metaboliti ndogo zisizotambulika). Kinyesi (16%) |
Vitambulisho | |
Nambari ya ATC | ? |
Data ya kikemikali | |
Fomyula | C14H18N6O |
| |
Data ya kimwili | |
Kiwango cha kuyeyuka | 165 °C (329 °F) |
(Hiki ni nini?) (thibitisha) |
Abacavir, inayouzwa chini ya jina la chapa Ziagen, ni dawa inayotumika kuzuia na kutibu HIV/UKIMWI.[1][2] Sawa na vizuizi vingine vya nucleoside analog reverse-transcriptase (NRTIs), abacavir hutumiwa pamoja na dawa zingine za HIV, na haipendekezwi yenyewe tu.[3] Inachukuliwa kwa mdomo kama tembe au kiowevu na inaweza kutumika kwa watoto zaidi ya umri wa miezi mitatu.[1][4]
Abacavir kwa ujumla inavumiliwa vizuri. [4] Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kutapika, shida ya kulala, homa na kuhisi uchovu.[1] Madhara yake makubwa zaidi ni pamoja na hisia kali(hypersensitivity), uharibifu wa ini na kuongezeka kwa asidi ya lactic mwilini (lactic acidosis).[1] Uchunguzi wa maumbile unaweza kuonyesha ikiwa mtu yuko katika hatari kubwa ya kupatwa na hisia kali (hypersensitivity).[1] Dalili za hisia kali ni pamoja na upele, kutapika na upungufu wa kupumua.[4] Abacavir iko katika kundi la dawa za NRTI, ambazo hufanya kazi kwa kuzuia nakala rudufu ya nyuma (reverse transcriptase), kimeng'enya kinachohitajika kwa ajili ya uzalishaji wa virusi vya HIV.[5] Ndani ya kundi la NRTI, abacavir ni nukleosidi ya karbosikliki (nucleoside ya carbocyclic).[1]
Abacavir ilipewa hati miliki mwaka wa 1988, na kuidhinishwa kutumika nchini Marekani mwaka wa 1998.[6][7] Iko kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Ulimwenguni.[8] Inapatikana kama dawa ya kawaida.[1] Gharama ya jumla katika nchi zinazoendelea kufikia mwaka wa 2014 ilikuwa kati ya dola za Marekani 0.36 na 0.83 kwa siku.[9] Kufikia mwaka wa 2016, gharama ya jumla kwa mwezi wa kawaida wa dawa nchini Marekani ni dola 70.50.[10] Kwa kawaida, abacavir huuzwa pamoja na dawa zingine za HIV, kama vile abacavir/lamivudine/zidovudine, abacavir/dolutegravir/lamivudine na abacavir/lamivudine.[4][5] Mchanganyiko wa abacavir/lamivudine pia ni dawa muhimu.[8]
Marejeleo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 "Abacavir Sulfate". The American Society of Health-System Pharmacists. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Agosti 2017. Iliwekwa mnamo 31 Julai 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Drug Name Abbreviations Adult and Adolescent ARV Guidelines". AIDSinfo. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-11-09. Iliwekwa mnamo 2016-11-08.
- ↑ "What Not to Use Adult and Adolescent ARV Guidelines". AIDSinfo. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-11-09. Iliwekwa mnamo 2016-11-08.
- ↑ 4.0 4.1 4.2 4.3 Yuen GJ, Weller S, Pakes GE (2008). "A review of the pharmacokinetics of abacavir". Clinical Pharmacokinetics. 47 (6): 351–71. doi:10.2165/00003088-200847060-00001. PMID 18479171.
- ↑ 5.0 5.1 "Nucleoside reverse transcriptase inhibitors (NRTIs or 'nukes') - HIV/AIDS". www.hiv.va.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-11-09. Iliwekwa mnamo 2016-11-08.
- ↑ Fischer, Janos; Ganellin, C. Robin (2006). Analogue-based Drug Discovery. John Wiley & Sons. uk. 505. ISBN 9783527607495. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Septemba 2017.
- ↑ Kane, Brigid M. (2008). HIV/AIDS Treatment Drugs. Infobase Publishing. uk. 56. ISBN 9781438102078. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Septemba 2017.
- ↑ 8.0 8.1 World Health Organization (2019). World Health Organization model list of essential medicines: 21st list 2019. Geneva: World Health Organization. hdl:10665/325771. WHO/MVP/EMP/IAU/2019.06. License: CC BY-NC-SA 3.0 IGO.
- ↑ "International Drug Price Indicator Guide". ERC. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Machi 2019. Iliwekwa mnamo 20 Novemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "NADAC as of 2016-12-07 | Data.Medicaid.gov". Centers for Medicare and Medicaid Services. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Desemba 2016. Iliwekwa mnamo 12 Desemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)