Siku ya Ukimwi duniani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Hii ni alama ya siku ya Ukimwi duniani
"Mpira" wa urefu wa mita 67 mjini Buenos Aires, Argentina, mojawapo ya mbinu za kampeni ya mwaka 2005 kwa Siku ya Ukimwi Duniani. Suala la kondomu linazidi kujadiliwa duniani kote.

Siku ya Ukimwi Duniani inaadhimishwa kila tarehe 1 Desemba kama siku maalumu ya kupanua ufahamu kuhusu maafa yanayoletwa na ugonjwa wa Ukimwi.

Desemba mosi ilichaguliwa kuwa siku ya Ukimwi kutokana na tarehe hiyo kuwa ndiyo siku ambayo virusi cha Ukimwi kilitambulika rasmi mwaka 1981. Toka mwaka 1981 hadi 2007 watu zaidi ya milioni 25 wameshafariki kutokana na Ukimwi. Mwaka 2007 peke yake walifariki milioni 2, kati yao watoto 270,000.

Siku hiyo ilichaguliwa rasmi mwaka 1988 wakati wa Mkutano wa Dunia wa Mawaziri wa Afya Kuhusu Mpango wa Kuzuia Ukimwi. Kuanzia hapo siku hiyo imekuwa ikikumbukwa rasmi na serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wanaharakati.

Toka mwaka 1988 hadi 2004, Siku ya Ukimwi Duniani ilikuwa ikiratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Ukimwi (UNAIDS). Mwaka 2005 UNAIDS ililipa shirika lisilo la kiserikali la Kampeni ya Ukimwi Duniani (the World AIDS Campaign) wajibu wa kuratibu siku hiyo.

Kila mwaka siku hiyo hufanyika kwa ujumbe maalumu. Ujumbe wa mwaka 2005 hadi mwaka 2010 ulikuwa, "Zuia Ukimwi: Timiza Ahadi".