Nenda kwa yaliyomo

Kisonono

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bakteria ya Neisseria gonorrhoeae, inayosababisha ugonjwa huu.
Dalili ya ugonjwa katika ngozi.
Dalili ya mtoto aliyezaliwa na mama mwenye kisonono.[1]

Kisonono (au kisalisali) ni maradhi ya zinaa ambayo husababishwa na bakteria wanaofahamika kisayansi kama Neisseria gonorrhoeae. Bakteria hao hushambulia utandotelezi unaozunguka sehemu za siri, lakini pia mdomo, macho na rektamu (puru).

Kama ilivyo klamidia, kisonono nacho huwa hakionyeshi dalili kila mara. Zikiwepo ni kama zile za klamidia ambazo huhusisha maumivu wakati wa kukojoa na ya chini ya kitovu kwa wanawake pamoja na kutokwa kwa majimaji yanayonuka au usaha mzito wa njano katika uke au uume. Dalili hixo hujitokeza siku 2 hadi 10 baada ya maambukizi.

Kisonono huonekana kwa urahisi kwa wanaume ambao hutoa usaha kutoka katika mfereji wa mkojo (urethra). Huanza kidogo, lakini huongezeka na huwa mwingi na kusababisha kusikia haja ya kukojoa mara kwa mara huku kukiwa na maumivu.

Kisonono kikisambaa na kufikia tezi kibofu, mfereji wa mkojo huziba kwa kiasi fulani. Kwa wanawake maambukizi hutokea katika urethra, uke au mlango wa uzazi (cervix). Ingawa mwasho unaotokana na majimaji katika uke unaweza kuwa mkubwa, mara nyingi dalili hizo ni chache au hamna kabisa katika hatua za awali.

Kisonono kisichotibiwa kinaweza kusababisha PID (Pelvic Infiammatory disease) kwa wanawake. Watoto wanaozaliwa na akina mama wenye kisonono huwa na hatari ya kuambukizwa wakati wa kuzaliwa; maambukizo hayo yanaweza kusababisha magonjwa ya meno kwa wachanga.

Utambuzi

[hariri | hariri chanzo]

Utambuzi wa ugonjwa hufanywa kwa kuchunguza usaha kutoka katika uke au uume au mkojo kwa uwepo wa Neisseria gonorrhoeae.

Kimataifa maambukizi yanakadiriwa kuwa milioni 88 kwa mwaka, mengi yakitokea Afrika na Asia Kusini. Wagonjwa ni 0.8% ya wanawake wote na 0.6% ya wanaume wote. Mwaka 2013 ugonjwa ulisababisha vifo 3,200.

Huko Marekani kisonono kiliongezeka kwa kiasi kikubwa mnamo miaka ya 1970 na mwanzoni mwa miaka ya 1980, hadi kukaribia kufikia kiwango cha magonjwa ya mlipuko kwa vijana wanaobalehe na watu wa umri wa kati. Ingawa kwa makisio maambukizi 360,000 ya kisonono huripotiwa kila mwaka nchini huko, wataalamu wamekisia kuwa watu 820,000 na zaidi huambukizwa bado kwa mwaka.

Kisonono hutibiwa kwa antibiotiki kadhaa, ingawa maambukizi yamekuwa na ukinzani juu ya tiba ya baadhi ya dawa katika miongo ya nyuma. Mwaka 2017 Shirika la Afya Duniani liliangalisha kuhusu baadhi ya bakteria hao kutodhibitika tena.

Moja kati ya mambo magumu katika kupambana na kisonono ni kutafuta mahusiano yote ya kimapenzi ya nyuma ya aliyeambukizwa ili kuweza kuzuia usambaaji zaidi wa ugonjwa.

  1. "Prophylaxis for Gonococcal and Chlamydial Ophthalmia Neonatorum in the Canadian Guide to Clinical Preventative Health Care" (PDF). Public Health Agency of Canada. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2010-03-10. Iliwekwa mnamo 2016-10-16. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kisonono kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.