Kuruka kamba
Mandhari
Kuruka kamba ni mchezo asilia wa watoto hasa. Kamba inashikwa kwa mikono na kuzungushwa juu ya kichwa na chini ya miguu. Kichocheo cha mchezo ni kuruka sawa wakati kamba inafika chini. Inachezwa katika nchi nyingi, pia katika Afrika ya Mashariki.
Kamba inaweza kushikwa na mtu mmoja au na wawili wanaoshika na kuruka pamoja. Njia nyingine ni kuwa na wawili wa kando wanaozungusha kamba na mmoja au wawili wanaoruka. Tena kuna namna tofauti za kushika kamba na namna tofauti za kuruka, kwa mfano miguu miwili kwa wakati mmoja, mguu mmoja tu au kwa kubadilishana mguu.
Katika nchi kadhaa ipo pia kama mchezo wa mashindano kufuatana na kanuni zilizokubaliwa.
Kuruka kamba hutumiwa pia na wanamichezo kama mazoezi ya kujenga nguvu.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kuruka kamba kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |