Rede
Rede ni mchezo asilia unaochezwa na Wanawake nchini Tanzania
Mchezo huu unashirikisha watu 20, 10 kwa kila timu. Walio mwishoni hurushiana mpira kwa kumlenga wa katikati. Huyo anakwepa kupigwa au huvizia kudaka mpira, kisha ampige nao mmojawao kati ya waliourusha. Akifaulu kumpiga alama huongezeka, la sivyo hupungua.
Umeanza kuchezwa zaidi na wanawake kuanzia miaka 15 toka miaka ya 1990; ulikuwa unachezwa na wanafunzi shuleni lakini kuanzia mwaka 2000 mchezo huu umekuwa na mvuto zaidi na kuchezwa na watu wazima na kila sehemu (mpaka mitaani).
Rede ina aina mbili, kuna rede ya chupa na rede ya mstari kati.
Timu ya Kwa Mkongo Queens ya Chamazi, Dar es Salaam, ndio mabingwa wa Mashindano ya Rede mstari kati maarufu kama T.O.K. REDE CUP 2021 na Ubingwa wa Mashindano ya Mbunge wa Mbagala, Mhe. Abdallah Chaurembo maarufu kama CHAUREMBO REDE CUP 2021/22.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Rede kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |