Tungo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Tungo ni neno au nomino inayotokana na kitenzi "tunga". Kutunga ni kuweka/kushikamanisha vitu pamoja kwa kutumia kitu kama kamba au uzi kwa kupitishia ndani yake. Kwa mfano, unaweza kutunga vitu kama samaki, shanga, simbi na kadhalika.

Unaposhikamanisha vitu pamoja tunapata kitu kinachoitwa utungo (mmoja) au tungo (nyingi).

Uchambuzi[hariri | hariri chanzo]

Katika taaluma ya lugha (sarufi) tuna dhana hiyohiyo ya kuweka/kushikamanisha vitu pamoja, yaani kupanga/kuweka pamoja vipashio vya lugha ili kujenga kipashio kikubwa zaidi.

Tungo ni nini?[hariri | hariri chanzo]

Neno tungo katika lugha ya Kiswahili, hasa kwa upande wa sarufi, lina maana ya neno au mpangilio wa maneno unaotoa taarifa fulani. Taarifa hiyo inaweza kuwa kamili au la. Mfano: Yeye anayesoma.... Yule anajua kuandika. Lakini lazima kuwe na mpangilio kamili katika muundo mzima wa kisarufi.

Aina za tungo[hariri | hariri chanzo]

Uainishaji wa tungo umejikita katika vigezo mbalimbali kutegemeana na matakwa ya mwainishaji. Baadhi ya vigezo vinaweza kutumika kwa kuainisha aina za tungo, nazo ni:

  1. Kigezo cha viwango
  2. Kigezo cha muundo
  3. Kigezo cha maana

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tungo kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.