Nenda kwa yaliyomo

Bradha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bradha Mfransisko

Bradha au bruda ni namna ya kutaja watawa wanaume Wakristo wasio makasisi. Maneno haya yamepokelewa katika Kiswahili kutoka Kiingereza "brother" au Kijerumani "Bruder".

Hali yake ya kuwekwa wakfu kwa kuahidi utekelezaji wa mashauri ya Kiinjili (ambayo ni hasa matatu: useja mtakatifu, ufukara na utiifu) inajitosheleza bila ya kuhitaji sakramenti maalumu.

Ni kama ilivyo kwa masista ambao katika Kanisa Katoliki na makanisa ya Kiorthodoksi hawawezi kupewa upadrisho.

Kwa kuwa lengo la utawa si kuongoza Kanisa kwa ile mamlaka inayotokana na Yesu na mitume wake kupitia daraja takatifu wala kutoa huduma za kipadri, bali ni kulenga utakatifu, yaani upendo kamili, kwa njia ya mkato.