Yohane Maria Vianney


Yohane Baptista Maria Vianney (Dardilly, 8 Mei 1786 – Ars-sur-Formans, 4 Agosti 1859), alikuwa padri mwanajimbo wa Kanisa Katoliki kutoka Ufaransa; kwa miaka zaidi ya 40 alifanya kwa namna ya ajabu kazi ya uchungaji kama paroko wa kijiji cha Ars, karibu na Belley, kwa kuhubiri mara nyingi, kusali na kufanya malipizi, huku sifa zake zikivutia watu kutoka nchi za nje ya Ulaya pia.
Kila siku katika katekesi aliyotoa kwa watoto na kwa watu wazima, katika upatanisho aliyowapatia walitobu na katika matendo yaliyojaa upendo wenye ari aliokuwa anauchota katika chemchemi ya ekaristi, alisonga mbele kiasi cha kueneza kila mahali mashauri yake na kusogeza kwa busara wengi kwa Mungu[1].
Alitangazwa na Papa Pius X kuwa mwenye heri tarehe 8 Januari 1905, halafu Papa Pius XI akamtangaza mtakatifu mwaka 1925 na msimamizi wa maparoko mwaka 1929.
Sala zake
[hariri | hariri chanzo]Nakupenda, Bwana, na neema pekee ninayokuomba, ni kwamba nikupende milele...
Mungu wangu, ikiwa ulimi wangu hauwezi kukariri kila nukta kwamba nakupenda, nataka moyo wangu ukuambie tena na tena kila ninapopumua.
Yesu wangu, jinsi inavyopendeza kukupenda!
Unijalie niwe kama wanafunzi wako juu ya mlima Tabori, nikikuona wewe tu, Mwokozi wangu.
Tuwe kama marafiki wawili ambao hata mmojawao hawezi kukubali kumchukiza mwingine. Amina.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo ya Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- Masomo ya Breviari - Sikukuu za Bwana, za Bikira Maria na za Watakatifu - Ndanda Mission Press 1978, uk 263-265
- John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 266-268
- Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 226-228
- Maurice Soseleje, Kalendari yetu – Maisha ya Watakatifu – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1986 – ISBN 9976-63-112-X, uk. 63
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- John Vianney--Cure d'Ars Ilihifadhiwa 17 Februari 2011 kwenye Wayback Machine.
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |
