Nenda kwa yaliyomo

Kalivari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Kalivari kadiri ya mapokeo ni ndani ya Kanisa la Kaburi na Ufufuo wa Yesu.
Altare iliyopo panaposadikiwa kuwa Golgotha. Wahiji wanainama na kubusu nyota inayoonyesha mahali ambapo, kadiri ya mapokeo msalaba wa Yesu ulisimamishwa.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Yesu
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho  • Utoto wa Yesu  • Ubatizo
Arusi ya Kana • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu  • Miujiza ya Yesu
Kugeuka sura • Karamu ya mwisho • Msalaba wa Yesu  • Maneno saba
Kifo cha Yesu  • Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  • Ujio wa pili
Injili  • Majina ya Yesu katika Agano Jipya  • Yesu kadiri ya historia  • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Ndugu wa Yesu • Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa

Kalivari au Golgotha ni mahali mjini Yerusalemu panaposadikiwa Yesu alisulubiwa na kuzikwa.

majina hayo mawili yana maana moja: mahali pa fuvu la kichwa, ambapo paliitwa hivyo kutokana na sura ya mwinuko wake.

Jina la pili ni jina la Kiaramu lilivyotoholewa katika Kigiriki (Γολγοθᾶ[ς], Golgotha[s], kutoka golgolta; kwa Kiebrania gulgōleṯ), la kwanza ni tafsiri ya Kilatini (Calvariæ Locus, kutoka ufafanuzi wa neno asili uliotolewa na wainjili Marko na Mathayo: Κρανίου Τόπος, Kraníou Tópos).

Zamani za Uyahudi ya Kale na Roma ya Kale sehemu ya kuua wakosaji ilikuwa nje ya mji wenyewe. Injili ya Yohane 19:20 inaeleza mahali palikuwa "nje ya mji", yaani nje ya ukuta wa mji wakati ule. Waraka kwa Waebrania 13:12 unataja "nje ya lango" [1].

Mapokeo ya karne ya 3 yalisema ni ndani ya sehemu ambako Kanisa la Kaburi na Ufufuo wa Yesu lilijengwa, maana kufuatana na mapokeo hayo kaburi lilikuwa karibu na Golgotha. Leo hii eneo linapatikana ndani ya ukuta wa mji wa kale uliopo uliojengwa katika karne ya 16.

  1. Kigiriki asilia ni "ἔξω τῆς πύλης" ekso tes pyles, tafsiri ya Biblia Habari Njema inatumia "nje ya mji"

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kalivari kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.