Marie Curie

Maria Curie (jina kamili: Maria Skłodowska-Curie;alizaliwa tar 7 Novemba alikufa tar 1867 – 4 Julai 1934) alikuwa mwanafizikia na mwanakemia Mpoland na Mfaransa aliyepata Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka 1903 na Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka 1911.
Alizaliwa Poland kama Maria Skłodowska wakati nchi hiyo ilipokuwa chini ya Urusi. Wakati ule hapakuwa na nafasi kwa wanawake kusoma kwenye chuo kikuu nchini, hivyo akahamia Ufaransa mwaka 1891 akajiandikisha katika somo la fizikia akaendelea baadaye kuchukua digrii ya hisabati.
Mwaka 1895 akaolewa na mwanasayansi Mfaransa Pierre Curie. Pamoja naye alifanya utafiti za unururifu akatambua elementi za poloni na radi.
Marie Curie ni binadamu pekee aliyepokea tuzo ya Nobel kwa sayansi mbili tofauti. Baadaye alikuwa profesa wa kike wa kwanza katika chuo kikuu cha Sorbonne mjini Paris.
Alikufa kutokana na kansa ya damu (au leukemia) kwa sababu alishika dutu nururifu nyingi maishani mwake bila ya tahadhari wakati hatari za unururifu hazijajulikana.
Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]
- 1903 Nobel Prize in Physics and 1911 Nobel Prize in Chemistry – Tovuti ya kamati ya Tuzo ya Nobel kwa Kiingereza
- Wasifu wa Curie
- The official web page of Maria Curie Skłodowska University in Lublin, Poland (Kiingereza)
![]() |
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Marie Curie kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |