Lanthanidi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Namba atomia Elementi ya kikemia Alama Picha
57 Lanthani La
58 Ceri Ce
59 Praseodimi Pr
60 Neodimi Nd
61 Promethi Pm
62 Samari Sm
63 Europi Eu
64 Gadolini M-ngu
65 Terbi Tb
66 Disprosi Dy
67 Holmi Ho
68 Erbi Er
69 Thuli Tm
70 Ytebi Yb
71 Luteti Lu

Lanthanidi au lanthanoidi (Kiingereza: lanthanides au lanthanoids) ni kundi la elementi za kimetali zenye namba atomia kutoka 57 hadi 71, ambazo tabia zake zinafanana. Elementi hizo huhesabiwa kati ya madini adimu kama vile monaziti. Kundi hilo huanza na lanthani na kuishia kwa luteti. [1] [2]

Lanthanidi ni metali zinazofanana katika tabia nyingi. Nyingi hubadilika polepole kuwa hidroksidi zake wakati zimewekwa ndani ya maji, sawa na metali alikali.

Hewani huunda kwa kawaida ganda jembamba la oksidi wakati sawa na metali nyingi. Lanthanidi, pamoja na skandi na ytri, huhesabiwa kati ya elementi za ardhi adimu. Lanthanidi zote ni metali nyeupe na laini zinazobadilisha rangi ya nje haraka zikiathiriana na hewa. Ugumu wake huongezeka sambamba na namba atomia.

Lanthanidi hazipatikani wala hazichimbwi kwa viwango vikubwa.

Matumizi[hariri | hariri chanzo]

Zina matumizi katika teknolojia mbalimbali kama vile:

  • Ceri: hutumiwa kama "jiwe la kibiriti" katika vibiriti vya gesi; pia kama kichocheo katika pirolisisi
  • Disprosi: hutumiwa kufyonza nyutroni ndani ya tanuri nyuklia
  • Erbi: imo katika filta za kupiga picha
  • Europi: hutumiwa kufyonza nyutroni ndani ya tanuri nyuklia, lakini pia kwa kuwasha rangi nyekundu katika skrini ya runinga
  • Gadolini: hutumiwa kuwasha rangi kibichi katika skrini ya runinga
  • Holmi: hutumiwa katika aloi; kwa jumla lanthanidi mbalimbali hutumiwa kama sehemu za aloi maana zinasaidia feleji kuwa nyumbufu zaidi wakati wa kuipa umbo
  • Luteti: kichocheo katika pirolisisi
  • Neodimi: huhitajika kwa sumaku kali; pia sehemu ya vioo vya miwani ya kinga cha mtia weko, hutumwa pia katika leza.
  • Praseodimi: katika kioo njano, k.v. kwa miwani ya kinga cha mtia weko
  • Promethi: ikiwa ni nururifu hutumiwa kama chanzo cha nishati kwa satelaiti na vipimaanga
  • Samari: kama sumaku ya kudumu, mfano katika kipaza sauti
  • Terbi: kwa leza
  • Thuli: kufyonza nyutroni ndani ya tanuri nyuklia
  • Yterbi: hutoa eksirei ilhali haihitaji umeme, mfano katika mashine za eksirei za kubeba

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lanthanidi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.