Nenda kwa yaliyomo

Seaborgi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Seaborgi (seaborgium)
Jina la Elementi Seaborgi (seaborgium)
Alama Sg
Namba atomia 106
Mfululizo safu Metali ya mpito
Uzani atomia 269
Valensi 2, 8, 18, 32, 32, 12, 2
Densiti 35 g/cm³ (kadirio)
Ugumu (Mohs) --
Asilimia za ganda la dunia 0 % (elementi sintetiki)
Hali maada inaaminiwa ni mango
Mengineyo tamburania, nururifu

Seaborgi (kwa Kiingereza: seaborgium) ni elementi sintetiki iliyo na alama Sg na namba atomia 106. Imepokea jina lake kwa heshima ya mwanakemia wa Marekani Glenn T. Seaborg . Ilhali ni elementi sintetiki, haitokei kiasili katika mazingira yetu lakini inaweza kuundwa katika maabara. Ni dutu nururifu; isotopi yake iliyo thabiti zaidi inaitwa 269 Sg, ikiwa na nusumaisha ya dakika 14 hivi.

Atomu za kwanza za seaborgi zilitengenezwa mwaka 1974 katika maabara huko Umoja wa Kisoyeti na Marekani. Pande hizo mbili zilivutana kwa miaka kadhaa kuhusu nani aliwahi kuigundua na haki ya kuamulia jina, hadi mwaka 1997 Jumuiya ya Kimataifa ya Kemia (IUPAC) iliamua jina rasmi kuwa "seaborgium".

Tabia nyingi za elementi hiyo hazijulikani kwa sababu mbili

a) elementi hii inapatikana tu baada ya kutengenezwa katika maabara kwa gharama kubwa [1]

b) baada ya kupatikana inaachana haraka, haidumu

Elementi 106 ilipewa jina la Glenn T. Seaborg, mtafiti wa elementi sintetiki, kwa jina seaborgium (Sg).

[2]

Marejeo

  1. Subramanian, S. "Making New Elements Doesn't Pay. Just Ask This Berkeley Scientist". Bloomberg Businessweek. Iliwekwa mnamo 2020-01-18.
  2. Barber, Robert C.; Gäggeler, Heinz W.; Karol, Paul J.; Nakahara, Hiromichi; Vardaci, Emanuele; Vogt, Erich (2009). "Discovery of the element with atomic number 112 (IUPAC Technical Report)". Pure and Applied Chemistry. 81 (7): 1331. doi:10.1351/PAC-REP-08-03-05.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Seaborgi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.