Nenda kwa yaliyomo

Bismuthi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Bismuthi (bisemutum; kiing. Bismuth)
Jina la Elementi Bismuthi (bisemutum; kiing. Bismuth)
Alama Bi
Namba atomia 83
Mfululizo safu Metali
Uzani atomia 208.980
Valensi 2, 8, 18, 32, 18, 5
Densiti 9.78 g/cm³
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 544.7 K (271.5  °C)
Kiwango cha kuchemka 1837 K (1564°C)
Asilimia za ganda la dunia 2 · 10-5 %
Hali maada mango
Mengineyo nururifu kidogo; Bismuthi tupu ina umbo la fuwele

Bismuthi ni elementi nururifu yenye namba atomia ya 82 kwenye mfumo radidia na uzani atomia ni 209.980. Jina latokana katika lugha ya Kijerumani lakini maana hayajulikani tena.

Tabia[hariri | hariri chanzo]

Ni metali nzito na kechu yenye rangi nyeupe-nyekundu lakini inaonekana kwa rangi mbalimbali. Tabia zake hufanana na antimoni na asenia lakini si sumu vile.

Mwaka 2003 imetambuliwa kuwa Bismuthi ni nurufifu kidogo. Lakini nusumaisha yake ni takriban miaka trilioni 19 hivyo haina hatari kwa binadamu.

Matumizi[hariri | hariri chanzo]

Hutumiwa kwa madawa ya vipodozi na madawa ya kiganga. Bismuthi imechukua nafasi ya metali ya risasi katika madawa kwa sababu si sumu. Kuna pia matumizi katika teknolojia mbalimbali.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bismuthi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.