Praseodimi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Praseodimi
Praseodimi (ikitunzwa ndani ya gesi ya Arigoni)
Praseodimi (ikitunzwa ndani ya gesi ya Arigoni)
Jina la Elementi Praseodimi
Alama Pr
Namba atomia 59
Mfululizo safu Lanthanidi
Uzani atomia 140.907
Valensi 2, 8, 18, 21, 8, 2
Densiti 6.475 g/cm3
Kiwango cha kuyeyuka 1208 K (935 °C)
Kiwango cha kuchemka 3403 K (3130 °C)
Asilimia za ganda la dunia 5,2 ppm
Hali maada mango

Praseodimi ni elementi ya kikemia yenye alama Pr kwenye jedwali la elementi. Inayo namba atomia 59 ambayo inamaanisha ina protoni 59 ndani ya atomu. Ni metali laini yenye rangi ya kifedha-kijivu, chumvi zake ni njano-kijani. Huhesabiwa kati ya Lanthanidi na metali za ardhi adimu.

Inachanganywa na magnesi kutengeneza aloi thabiti kwa ajili ya matumizi ndani za injini za eropleni. Inaweza pia kutumiwa kutia rangi ya kijani kibichi kwenye vioo.

Praseodimi ilitengwa kwanza na madini mengine mnamo 1885 na mwanakemia wa Austria Carl Auer von Welsbach. Inapatikana katika mchanga, unaoitwa mchanga wa monaziti, huko Marekani (Florida, Kalifornia), Uhindi, na Brazil.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Praseodimi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.