Magnesi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Magnesi (Magnesium)
Jina la Elementi Magnesi (Magnesium)
Namba atomia 12
Mfululizo safu Metali za udongo alkalini
Uzani atomia 24,305 u
Valensi 2, 8, 2
Ugumu (Mohs) 1–2.5
Kiwango cha kuyeyuka 923 K (650 °C)
Kiwango cha kuchemka 1380 K (1107 °C)

Magnesi (pia magnesiamu) ni elementi na metali ya udongo alkalini yenye namba atomia 12 kwenye mfumo radidia ina uzani atomia 24.3050. Alama yake ni Mg. Jina linahusiana na neno la Kigiriki μαγνησιη (magnesia - sumaku) hata kama Mg haina tabia za kisumaku.

Elementi tupu ina valensi mbili na rangi yake ni nyeupe-fedha. Mg ni kati ya elementi zinazopatikana kwa wingi duniani ikiwa na nafasi ya nane na asilimia 1.4 za ganda la dunia ni magnesi.

Inamenyuka kwa urahisi kikemia, hivyo haitokei kama elementi tupu lakini kwa kampaundi mbalimbali, hasa katika magnesiti, dolomiti na madini mengine. Katika maji ya bahari iko kwa kiwango cha kg 1 kwa kila .

Unga wa magnesi au vipande vidogo vya metali huungua moto mkali mweupe, unga hata bila kuwashwa hewani tu.

Magnesi ni muhimu kwa miili ya wanadamu na wanyama, pia kwa mimea. Wanamichezo hutumia mara nyingi dawa ya magnesi wakitaka kuboresha mbio au kuongezewa nguvu.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Magnesi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.