Nenda kwa yaliyomo

Neodimi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Neodimi
Jina la Elementi Neodimi
Alama Nd
Namba atomia 60
Mfululizo safu Lanthanidi
Uzani atomia 144.242
Valensi 2, 8, 18, 22, 8, 2
Densiti 7.01 g/cm3
Kiwango cha kuyeyuka 1297 K (1024 °C)
Kiwango cha kuchemka 3347 K ​(3074 °C)
Sumaku ya aloi ya neodimi inayotumiwa ndani ya diski kuu ya kompyuta

Neodimi (Neodymium) ni elementi na metali ya udongo adimu yenye namba atomia 60 kwenye jedwali la elementi maana yake kuna protoni 60 katika kiini cha atomu yake. Ina uzani atomia 144.242. Alama yake ni Nd.

Neodimi inaitwa "metali ya udongo adimu", hata hivyo si elementi haba Duniani. Kama metali zote inang'aa lakini hewani inaoksidishwa haraka na kupata ganda la oksidi. Kutokana na kuoksidisha haraka inaanza kuwaka ikifikia sentigredi 150 na kuwa oksidi ya Nd2O3.

Aloi ya Nd2Fe14B) ni sumaku yenye nguvu sana: inashinda sumaku nyingine zote. Sumaku ya neodimi inaweza kushika masi yake mara elfu.

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Kwa hiyo matumizi yake ni hasa pale ambako sumaku nyepesi lakini yenye uwezo inahitajika. Kwa hiyo zinatafutwa kwa ajili ya kompyuta, vinasasauti au vipazasauti.

Katika karne ya 21 uhandisi wa injini mpya za umeme kwa ajili ya magari na eropleni ulipanua matumizi ya neodimi. Kwa mfano injini za umeme za gari la Toyota Prius zinahitaji kilogramu moja ya neodimi kwa kila gari. [1] Mwaka 2018 kampuni ya Tesla ilihamia pia matumizi ya neodimi [2].

  1. As hybrid cars gobble rare metals, shortage looms , taarifa ya Reuters ya August 31, 2009, alitazamiwa Machi 2018
  2. Tesla's electric motor shift to spur demand for rare earth neodymium, tovuti ya Reuters ya March 12, 2018, iliangaliwa Machi 2018
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Neodimi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.