Kinasasauti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kinasasauti ya miaka ya 55s

Kinasasauti (pia mikrofoni au maikrofoni kutoka lugha ya Kiingereza: microphone) ni kifaa kinachoweza kuichukua sauti na kuibadili ili iwe ishara za umeme (electrical signals).

Kinasasauti hutumika katika simu, vifaa vinavyosaidia watu walio na shida za kusikia, pamoja na vifaa vya kuhadhiri kwa watu wengi katika jukwaa na ukumbi. Unapoongea kwa kinasasauti, ile sauti hufanywa kubwa na baadaye kusikika kwa kipaza sauti. Kinasasauti pia hupatikana katika studio za kurekodi muziki ambapo mtu hukitumia na ile sauti huhifadhiwa kwa tarakilishi na baadaye kuhaririwa ili muziki utolewe. Kwa leo, hili ni jambo la kawaida haswa kwa wale wanaotengeneza video za youtube ili sauti yao iwe ya kuvutia na kusikika kwa urahisi.

Historia ya kinasasauti[hariri | hariri chanzo]

Ilifika pahali katika historia ambapo watu walihitaji kuifanya sauti yao iwe kubwa kuliko kawaida. Waigizaji na waimbaji katika kumbi za michezo waliona kwamba sauti zao hazisikiki vizuri na kwa hiyo wakaanza kutumia vinasasauti vilivyofanana na honi ya baiskeli.

Mvumbuzi Robert Hooke ndiye aliyekuwa wa kwanza kujaribu kutumia kinasasauti kilichofunganishwa na uzi kilichojulikana kama lover's telephone.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]