Kipaza sauti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

kinasasauti

Kipaza sauti: Mwendo wa sumaku (nyekundu) unasababisha mitetemo ya utando ndani yake (A) inayoendelea kama mitetemo ya hewa nje yake (B) inayofika kwenye sikio kama sauti
Kipaza sauti ya kawaida yenye utando wa karatasi ngumu

Kipaza sauti ni kifaa kinachotoa sauti kwenye redio, runinga au ala za muziki ya elektroniki. Kifaa hiki kina uwezo wa kupaza sauti asilia na hapo asili ya jina lake.

Misingi ya kipaza sauti[hariri | hariri chanzo]

Inapokea mishtuko ya umeme na kuibadilisha kuwa mwendo wa sumaku ndogo ndani yake inayosogea mbele na nyuma. Sumaku inaunganishwa na mtando wa kipaza sauti na kuitetemesha kwa miendo yake. Mitetemo ya utando ndani ya kipaza sauti inaendelea kama mitetemo ya hewa mbele ya utando. Mitetemo inasambaa na kupokelewa na kiwambo cha sikio kama sauti.

Kinyume cha kipaza sauti ni kinasasauti (microphone) inayopokea mitetemo ya sauti kwa utando ndani yake na kuzibadilisha kuwa mishtuko ya umeme inayoweza kupokelewa tena na kipaza sauti.