Holmi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Holmi (Holmium)

Jina la Elementi
Holmi (Holmium)
Alama Ho
Namba atomia 67
Mfululizo safu Lanthanidi
Uzani atomia 164.930
Valensi 2, 8, 18, 29, 8, 2
Densiti 8.79 g/cm3
Kiwango cha kuyeyuka °K 1734
Kiwango cha kuchemka °K 2873

Holmi (Holmium) ni elementi ya kimetali yenye alama Ho na namba atomia 67, maana yake kiini cha Holmi kina protoni 67 ndani yake. Uzani atomia ni 164.930[1]. Katika jedwali la elementi inahesabiwa kati ya lanthanidi na metali za ardhi adimu.

Holmi ilitambuliwa kama elementi ya pekee nchini Uswidi na mwanakemia Per Theodor Cleve kwenye mwaka 1878. Aliikuta kama taka ndani ya oksidi ya Erbi, pamoja na Thuli. Cleve alichagua jina la Holmi kwa heshima ya mji Stockholm alikozaliwa. [2] [3] [4]

Holmi safi ni metali laini. Kiasili Holmi haipatikani kwa hali safi kwa sababu inatendana kirahisi na kemikali nyingine. Lakini inapatikana ndani ya madini monaziti na gadoliniti.[5] Maeneo makuu ya madini ni China, Marekani, Brazil, Uhindi, Sri Lanka, na Australia na akiba ya holmi inakadiriwa kuwa tani 400,000. [6]

Baada ya kusafishwa inakaa katika hewa kavu kwa halijoto ya kawaida. Ikifikia nyuzijoto °C 150 inawaka.

Holmi huwa na nguvu kubwa ya usumaku, na hapo inapita elementi zote nyingine. Kwa sababu hiyo hutumiwa kuzalisha sumaku zenye nguvu kuu. [7]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Meija, Juris; et al. (2016). "Atomic weights of the elements 2013 (IUPAC Technical Report)". Pure and Applied Chemistry. 88 (3): 265–91. doi:10.1515/pac-2015-0305
  2. Marshall, James L. Marshall; Marshall, Virginia R. Marshall (2015). "Rediscovery of the elements: The Rare Earths–The Confusing Years". The Hexagon: 72–77. Retrieved 30 December 2019. 
  3. Holmium. Royal Society of Chemistry (2020). Iliwekwa mnamo 4 January 2020.
  4. Stwertka, Albert (1998). A guide to the elements (2nd ed.). Oxford University Press. p. 161. ISBN 0-19-508083-1. 
  5. Hudson Institute of Mineralogy (1993–2018). Mindat.org. www.mindat.org. Iliwekwa mnamo 14 January 2018.
  6. John Emsley (2001). Nature's building blocks: an A-Z guide to the elements. US: Oxford University Press. pp. 181–182. ISBN 0-19-850341-5. 
  7. R. W. Hoard; S. C. Mance; R. L. Leber; E. N. Dalder; M. R. Chaplin; K. Blair et al. (1985). "Field enhancement of a 12.5-T magnet using holmium poles". IEEE Transactions on Magnetics 21 (2): 448–450. Bibcode:1985ITM....21..448H. doi:10.1109/tmag.1985.1063692. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Holmi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.