Nenda kwa yaliyomo

Ytri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ytri



Ytri
Jina la Elementi Ytri
Alama Y
Uzani atomia 88.90585 u
Valensi 2, 8, 18, 9, 2
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 1799 K (1526 °C)
Kiwango cha kuchemka 3609 K (3336 °C)

Ytri ni elementi na metali yenye kifupi Y na namba atomia 39 katika mfumo radidia.

Kiasili haipatikani kama elementi peke yake ila tu katika hali ya kampaundi na elementi mbalimbali. Baada ya kutolewa katika mchanganyiko na kusafishwa rangi yake ni nyeupe-kifedha.

Matumizi yake ni hasa kwa rangi nyekundu katika mitambo kama neli zinazoonesha rangi katika skrini cha televisheni au cha kompyuta.

Jina limetokana na kijiji cha Ytterby nchini Uswidi ambako ilitambuliwa mara ya kwanza.[1].

  1. Elementi nne zilipokea majina yake kutokana na kijiji hicho ambako madini yake yalipatikana na kuchunguliwa: Ytri (Yttrium), Terbi (Terbium), Yterbi (Ytterbium) na Erbi (Erbium)
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ytri kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.