Nenda kwa yaliyomo

Ytterby

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Terbiumvägen (terbium Road) na Gruvvägen (Mine Road) karibu na mgodi Ytterby ( 59°25′42″N 18°21′14″E / 59.42836°N 18.35384°E / 59.42836; 18.35384 (Terbiumvägen / Gruvvägen) )

Ytterby ni kijiji kwenye kisiwa cha Resarö, katika Manispaa ya Vaxholm kwenye funguvisiwa la Stockholm nchini Uswidi.

Jina la kijiji linamaanisha "kijiji cha nje". [1] Ytterby ni maarufu kwa sababu katika migodi yake elementi nane zilitambuliwa mara ya kwanza. Elementi nne za Ytri (Y), Yterbi (Yb), Erbi (Er) na Terbi (Tb) zote zimepewa jina la Ytterby.

Ugunduzi wa elementi

[hariri | hariri chanzo]

Tangu miaka ya 1500 hivi felspar ilichimbwa hapa kwa ajili ya kiwanda cha kauri. Mnamo 1787 luteni Carl Axel Arrhenius aliyechungulia eneo kwa kupata mahali pa kujenga ngome alikuta jiwe jeusi na zito ambalo halikujalikana. [2] Mwaka 1794 jiwe hilo lilifanyiwa utafiti na mtaalamu Johan Gadolin aliyetambua kwamba sehemu kubwa ilikuwa elementi mpya. Mwanakemia wa Uswidi Anders Gustaf Ekeberg alithibitisha ugunduzi huo mwaka uliofuata na akaiita kwa jina la Yttria, na yale madini aliitwa Gadoliniti. [3]

Ndani ya madini ya gadoliniti jumla ya elementi saba ilipatikana.

Mbali na Ytri (Y), Yterbi (Yb), Erbi (Er) na Terbi (Tb), elementi za Scandi (Skandinavia), Holmi (Ho, jina la Stockholm), Thuli (Tm, jina la Thule, kisiwa cha kaskazini katika mitholojia ya Kigiriki) ya Scandinavia), na Gadolini (Gd, jina la mvumbuzi Johan Gadolin) zilitambuliwa katika madini ya Ytterbi. [4]

  1. Emsley, John (2001). Nature's Building Blocks. Oxford University Press. uk. 496. ISBN 0-19-850341-5.
  2. Knutson Udd, Lena (2012). "Ytterby gruva" (PDF) (kwa Swedish). Fortifikationsverket. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (pdf) mnamo 2018-01-07. Iliwekwa mnamo 6 Januari 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link)
  3. Krishnamurthy, Nagaiyar (2015). Extractive Metallurgy of Rare Earths (tol. la 2nd). CRC Press. ku. 2, 839. ISBN 9781466576384.
  4. Kean, Sam (16 Julai 2010). "Ytterby: The Tiny Swedish Island That Gave the Periodic Table Four Different Elements". Slate. Iliwekwa mnamo 14 Novemba 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Uswidi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ytterby kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.