Neoni
Jump to navigation
Jump to search
Neoni (Neon) | |
---|---|
| |
Jina la Elementi | Neoni (Neon) |
Alama | Ne |
Namba atomia | 10 |
Mfululizo safu | Gesi adimu |
Uzani atomia | 20.1797 |
Densiti | 0.9002 g/L |
Kiwango cha kuyeyuka | 24.56 K (-248.59 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 27.07 K (-246.08 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 5 · 10-7 % |
Hali maada | gesi |
Neoni (kut. kigiriki νέος neos - "mpya") ni elementi ya kikemia yenye namba atomia 10 na uzani wa atomi 20.1797. Alama yake ni Ne.
Duniani yapatikana katika angahewa kama gesi adimu na bwete isiyo na rangi wala ladha. Kwa sababu ya tabia yake ya ubwete kampaundi hazijulikani.
Neoni yapatikana kwa wingi katika anga ya ulimweguni lakini ni haba duniani. Ni gesi adimu nyepesi duniani baada ya heli.
Matumizi[hariri | hariri chanzo]
Neoni ikipitishwa na umeme yatoa mwanga mwekundu hivyo yatumiwa katika taa memetevu na matangazo memetevu.
Inatumiwa pia katika teknolojia ya friji kama kizizimshi.