Gesi adimu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Gesi adimu ni mfulizo wa kikemia katika mfumo radidia unaounganisha elementi za kundi la 18 yaani Heli (He), Neoni (Ne), Arigoni (Ar), Kriptoni (Kr), Xenoni (Xe) na Radoni (Rn).

Elementi hizi zote zapatikana kama gesi kwa hali sanifu; hazina rangi wala harufu; haziwaki.

Zapatikana katika hali ya atomi badala ya molekyuli yaani hazimenyuki. Sababu ya kutomenyuka ni tabia ya mizingo elektroni inayojaa yote kabisa kwa hiyo hakuna haja kuhamia hali thabiti zaidi; gesi hizi zimeshafikia kila atomi peke yake. Kwa hiyo hakuna kampaundi ya gesi hizi.

Gesi hizi zote ziko hewani lakini kwa kiasi kidogo tu. Radoni pekee yake ni hatari ya binadamu laki i si kwa sababu ya tabia zake za kikemia bali na tabia yake ya kifizikia kwa sababu radi ni elementi mnururishi.