Nenda kwa yaliyomo

Cadimi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Cadimi au Kadimi (Cadmium)
Kipande cha Cadimi
Kipande cha Cadimi
Jina la Elementi Cadimi au Kadimi (Cadmium)
Alama Cd
Namba atomia 48
Mfululizo safu Metali ya mpito
Uzani atomia 102.9055
Valensi 2, 8, 18, 18, 2
Densiti 112.411 g/cm³
Ugumu (Mohs) 2.0
Kiwango cha kuyeyuka 594.22 K (321.07 °C)
Kiwango cha kuchemka 1040 K (767 °C)
Asilimia za ganda la dunia 10-5
Hali maada mango
Mengineyo metali haba

Cadimi (pia: Kadimi - kupitia Kilatini "Cadmium" kutoka Kigiriki καδμεία kadmeia iliyotaja mitapo yenye cadimi kwa heshima ya mungu wa Kigiriki Κάδμος Kadmos) ni elementi na metali haba duniani. Kikemia ni elementi ya mpito yenye kifupi cha Cd na namba atomia 48 katika mfumo radidia.

Tabia na matumizi[hariri | hariri chanzo]

Cadimi ni metali laini yenye rangi nyeupe-buluu. Hufanana mara nyingi na tabia za zinki lakini humenyuka kwa urahisi zaidi. Cadimi yenyewe na kampaundi zake huwa sumu na kusababisha kansa.

Matumizi yake ni hasa katika betri na viungo vya rangi. Kwa teknolojia ya kinyuklia hutumiwa kama kinga dhidi ya nyutroni katika matanuri ya nyuklia.

Nondo za Cadimi zilitumiwa na Enrico Fermi mwaka 1942 katika tanuri nyuklia ya kwanza kwa kusudi la kutawala mmenyuko mfulizo wa nyuklia. Nondo hizo zilisukumwa kati ya nondo za urani na kupunguza mwendo wa nyutroni kati ya nondo za urani.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Cadimi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.