Sulfuri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search


Sulfuri (salfa, kibiriti)
Sulfuri ikiwaka yayeyuka kuwa kiowevu chekundu; rangi ya moto ni buluu.
Sulfuri ikiwaka yayeyuka kuwa kiowevu chekundu; rangi ya moto ni buluu.
Jina la Elementi Sulfuri (salfa, kibiriti)
Alama S
Namba atomia 16
Mfululizo safu Simetali
Uzani atomia 32.065
Kiwango cha kuyeyuka 388.36 K (115.21 °C)
Kiwango cha kuchemka 717.8 K (444.6 °C)
Asilimia za ganda la dunia 0.05 %
Hali maada imara

Sulfuri (pia salfa au kibiriti) ni elementi simetali yenye namba atomia 16 kwenye mfumo radidia na uzani atomia 32.065. Alama yake ni S. Kwenye hali sanifu ni imara kuwa fuwele zenye rangi ya njano.

Kutokea duniani[hariri | hariri chanzo]

Hutokea duniani kama elementi tupu hasa kwenye volkeno lakini zaidi kwenye kampaundi ndani ya madini ya sulfidi. Leo hii inapatikana kutokana na mafuta ya petroli wakati yakisafishwa.

Sulfuri ni elementi ya lazima kwa maada hai na seli zote zatumia sulfuri.

Matumizi ya kibiashara[hariri | hariri chanzo]

Matumizi yake ya kibiashara ni hasa kwa mbolea wa chumvi, lakini pia katika baruti, viberiti na madawa ya wadudu.

Sulfuri - kibiriti[hariri | hariri chanzo]

Jina jingine la sulfuri ni "kibiriti" (Kar. كبريت) linalopatikana kwa mfano katika tafsiri za Biblia (k.m. Luka 17,29, Ufunuo 9,17). Matumizi ya neno hili kwa ajili ya "vibiriti" yalijitokeza kwa sababu mwanzoni kichwa cha vijiti kilikuwa na mchanganyiko wa madawa yenye sulfuri au "kibiriti" ndani yake. Hivyo tafsiri nyingine ya "vibiriti" ni "vijiti vyenye sulfuri".


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Chem template.svg Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sulfuri kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.