Kibiriti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kwa elementi ya kikemia tazama sulfuri
Vibiriti vya vijiti
Kibiriti cha gesi

Kibiriti (kutoka Kar. كبريت kibrit) ni kifaa cha kuwashia moto.

Maana asilia: elementi[hariri | hariri chanzo]

Kiasili neno lataja elementi ya rangi njano inayoitwa zaidi sulfuri kwa jina la kikemia. Kwa maana hiyo neno lapatikana katika Biblia kwa mfano Ufunuo 9.17.

Vijiti vya sulfuri au kibiriti[hariri | hariri chanzo]

Dawa la kiberiti au sulfuri latumiwa pia kwa vijiti vya kuwashia moto na hivyo neno "kibiriti" limepata maana yake ya kawaida. Kichwa cha kuwaka kina sulfuri ndani yake pamoja na posferi.

Kibiriti cha gesi au petroli[hariri | hariri chanzo]

Jina la kibiriti latumiwa pia kwa ajili ya vifaa vinavyowacha moto hata kama hakuna kibiriti chenyewe au sulfuri ndani yao. Siku hizi ni kama chombo kidogo chenye gesi ndani yake pamoja na mtambo wa kutengeneza kimota cha kuwashia gesi. Kuna aina ya bei ya duni inayotupwa baada ya gesi kukwisha na aina nyingine inayojaziwa upya.

Kuna pia aina nyingine inayotumia petroli pamoja na utambi.