Nenda kwa yaliyomo

Protaktini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Protaktini (Protaktinium)
Protaktini katika mfumo radidia
Protaktini katika mfumo radidia
Jina la Elementi Protaktini (Protaktinium)
Alama Pa
Namba atomia 91
Mfululizo safu Aktinidi
Uzani atomia 231.04
Valensi 2, 8, 18, 32, 20, 9, 2
Densiti 15.37 g/cm³
Kiwango cha kuyeyuka °K 1841
Kiwango cha kuchemka °K 4300
Asilimia za ganda la dunia ppm 9 · 10−8
Hali maada mango
Mengineyo nururifu

Protaktini (protactinium) ni elementi ya kimetali yenye alama Pa na namba atomia 91. Uzani atomia ni 231.04. Ni elementi haba sana isiyo na matumizi yoyote nje ya utafiti wa kisayansi.

Tabia muhimu[hariri | hariri chanzo]

Protaktini ina rangi ya kijivu-kifedha. Ni nururifu sana; kiasili kuna isotopi mbili kwa viwango vidogo sana; 231Pa huwa na nusumaisha ya miaka 32,000 na 234Pa yenye nusumaisha chini ya masaa saba. Zote mbili hutokea kiasili katika mbunguo nyuklia wa urani lakini kwa viwango vidogo kiasi kwamba Protaktini yote kwa utafiti hutolewa katika matanuri ya nyuklia.

Matumizi[hariri | hariri chanzo]

Kutokana na uhaba wake, unururifu mkubwa na uwezo wake wa kusumisha, kwa sasa hakuna matumizi ya protaktini nje ya utafiti wa kitaalamu.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Isotopi ya 234Pa iligunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Ujerumani mnamo 1913, kwenye mwaka ilipata jina lake kutoka Otto Hahn na Lise Meitner waliogundua isotopi ya 231Pa na kutambua inatokea "kabla ya Aktini" (proto-actinium) yaani walitambua kwamba elementi ya Aktini inazalishwa wakati wa mbunguo nyuklia wa hiyo elementi mpya.

Mnamo mwaka 1961 Mamlaka ya Nishati ya Nyuklia ya Uingereza ilizalisha gramu 125 za Antaktini safi kwa kusafisha tani 60 za taka nyuklia katika mchakato wa hatua 12 uliogharamia dolar 500,000. Kwa miaka mingi iliyofuata, akiba hii ilikuwa msingi wa majaribio yote duniani.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Tovuti za nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Protaktini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.