Thori

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Thori (Thorium)
Kipande kidogo cha bati cha Thori, iliyofungwa katika gesi ya Arigoni (inayozuia kuoksidika)
Kipande kidogo cha bati cha Thori, iliyofungwa katika gesi ya Arigoni (inayozuia kuoksidika)
Jina la Elementi Thori (Thorium)
Alama Th
Namba atomia 90
Mfululizo safu Aktinidi
Uzani atomia 232.0377
Valensi 2, 8, 18, 32, 18, 10, 2
Densiti 10 g/cm³ (kadirio)
Ugumu (Mohs) 3.0
Kiwango cha kuyeyuka °K 2023
Kiwango cha kuchemka °K 5061
Asilimia za ganda la dunia ppm 11
Hali maada mango
Mengineyo nururifu

Thori (thorium) ni elementi ya kimetali yenye alama Th na namba atomia 90.

Thori safi ni metali laini yenye rangi ya kifedha-kijivu; baada ya kukaa hewani inaelekea polepole kuwa nyeusinyeusi.

Iligunduliwa Norwei na kupewa jina lake Uswidi mwaka 1829. Jina la Thori limechukuliwa kutoka mungu wa ngurumu wa Skandivia ya Kale.

Thori ni elementi yenye unururifu dhaifu. Isotopi yake ya 232Th ina nusumaisha ya miaka bilioni 14.05 inayozidi hata umri wa Dunia. Wanajiolojia hukadiria kuwa mbunguo nyuklia wa Thori unachangia sana katika joto lililopo ndani ya Dunia[1].

Inapatikana kiasili katika madini, hasa Uhindi, Marekani na Australia. Akiba zake ni kubwa kushinda urani, kwa hiyo kuna majadiliano kama itafaa kutumiwa kwa tanuri nyuklia baada ya kumaliza akiba za urani[2]. Lakini kuna pia wasiwasi kwa sababu inaonekana si thabiti kama urani katika mchakato wa mwatuko nyuklia, hivyo kuna hofu ya ajali pamoja na hatari ya matumizi ya thori kutoka tanuri kwa ajili ya silaha za nyuklia[3].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Gando, A.; Gando, Y.; Ichimura, K.; et al. (2011). "Partial radiogenic heat model for Earth revealed by geoneutrino measurements" (PDF). Nature Geoscience. 4 (9): 647–651. Bibcode:2011NatGe...4..647K. doi:10.1038/ngeo1205.
  2. Thorium, tovuti ya World Nuclear Association (shirika la tasnia ya kinyuklia), iliangaliwa Machi 2020
  3. Stephen F. Ashley, Geoffrey T. Parks, William J. Nuttall, Colin Boxall, Robin W. Grimes: Thorium fuel has risks. In: Nature. Band 492, Nr. 7427, 6. Dezember 2012, S. 31–33, doi:10.1038/492031a

Tovuti za Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Thori kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.