Bromi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Bromi
Jina la Elementi Bromi
Alama Br
Namba atomia 35
Mfululizo safu Halojeni
Uzani atomia 79.904
Valensi 2, 8, 18, 7
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 265.8 K (-7.3 °C)
Kiwango cha kuchemka 332.0 K (58.8  °C)
Asilimia za ganda la dunia 6 · 104  %
Hali maada kiowevu

Bromi (pia bromini, kut. Kigiriki βρῶμος bromos "kunuka kwa wanyama" ) ni elementi yenye namba atomia 35 katika mfumo radidia maana yake kiini atomia chake kina protoni 35. Uzani atomia ni 79.904 na alama yake ni Br. Ni elementi ya tatu katika safu ya halojeni.

Katika hali sanifu ni kiowevu yenye rangi nyekundu kahawia. Inamenyuka haraka na elementi nyingine na kwa wanyama pia watu ni sumu.

Bromi yapatikana kwa wingi katika maji ya bahari.