Nenda kwa yaliyomo

Indi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Indi (Indium)
Waya ya Indi
Waya ya Indi
Jina la Elementi Indi (Indium)
Alama In
Namba atomia 49
Mfululizo safu Metali
Uzani atomia 114.818
Valensi 2, 8, 18, 18, 3
Densiti 7.31 g/cm³
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 429.75 K (156.60 °C)
Kiwango cha kuchemka 2345 K (2072 °C)
Asilimia za ganda la dunia 1 · 10-5 %
Hali maada mango
Mengineyo Isotopi ya kawaida ina kiwango kidogi cha unururifu

Indi ni elementi. Namba atomia yake ni 49 kwenye mfumo radidia na uzani atomia ni 114.818. Jina limepatikana kutoka kwa rangi ya indigo au buluu ya Kihindi katika taswirangi yake.

Ni metali haba na laini yenye rangi ya kifedha-nyeupe.

Hupatikana hasa katika mitapo za zinki.

Indi ina matumizi mengi ila tu kutokana na uhaba wake hutumiwa zaidi katika kampaundi si metali tupu. Siku hizi sehemu kubwa hutumiwa kwa umbo la oksidi ya indi katika skrini nyembamba za kompyuta na televisheni. Matumizi mengine ni ya kilainishaji ndani ya mashine.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Indi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.