Nenda kwa yaliyomo

Rubidi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Rubidi
(Rubidium)
Rubidi ndani ya tubu katika angahewa ya arigoni
Rubidi ndani ya tubu katika angahewa ya arigoni
Jina la Elementi Rubidi
(Rubidium)
Alama Rb
Namba atomia 37
Mfululizo safu Metali alikali
Uzani atomia 85.4678
Valensi 2, 8, 18, 8, 1
Densiti 1.532
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 312.46 K (39.31 °C)
Kiwango cha kuchemka 961 K (688 °C)
Asilimia za ganda la dunia 0.3 %
Hali maada mango

Rubidi (Kilat. rubidus: nyekundu) ni elementi na metali alikali yenye namba atomia 37 kwenye mfumo radidia na uzani atomia 85.4678. Alama yake ni Rb.

Tabia[hariri | hariri chanzo]

Kali (potasiamu) ni metali laini sana inayochemka kwa sentigredi 39 tayari. Rangi yake ni nyeupe-fedha. Haipatikana kiasili kama metali tupu kwa sababu humenyuka haraka na kuoksidika hewani. Inamenyuka vikali sana na oksijeni na kuwaka peke yake ikiwekwa hewani tu.

Rubidi hutokea kwa umbo la isotopi mbili; 85Rb ni thabiti lakini 87Rb ni mnururifu na kugeuka kuwa 87Sr. Lakini nusumaisha yake ni miaka bilioni 48 hivyo unururifu ni mdogo.

Matumizi[hariri | hariri chanzo]

Kutokana na uhaba wa metali kuina matumizi chache tu hasa katika utafiti wa kisayansi.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rubidi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.