Roentgeni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Roentgeni (Roentgenium)
Jina la Elementi Roentgeni (Roentgenium)
Alama Rg
Namba atomia 111
Mfululizo safu Simetali
Uzani atomia 280 u
Valensi 2, 8, 18, 32, 32, 18, 1
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Asilimia za ganda la dunia 0
Wilhelm Conrad Röntgen

Roentgeni (jina la awali hadi 2004: Unununium) ni elementi sintetiki yenye namba atomia 111 katika mfumo radidia na uzani atomia wa isotopi yake yenye nusumaisha ndefu ni 280. Alama yake ni Rg.

Roentgeni haitokei kiasili kwa sababu nusumaisha ya isitopi zake ni fupi mno. 272Rg ina nusumaisha ya sekunde 0.0038 pekee; isotopi yenye nusumaisha ndefu ya sekunde 3.6 ni 280Rg. Hadi sasa isotopi mbili nyingine zilitambiluwa zenye nusumaisha ya millisekunde 170 (279Rg) na 6.4 (274).

Roentgeni ilitambuliwa mara ya kwanza na wanasayansi wa taasisi ya utafiti wa kinyuklia huko Darmstadt. Walifaulu kuitengeneza katika chombo cha nyuklia mara sita pia watafiti Wajapan walifaulu mara chache. Jina limekubaliwa kimataifa kuwa "Roentgeni" kwa heshima ya Konrad Röntgen.

Kama elementi zote za sintetiki hazina matumizi zatengenezwa tu kwa kusudi la utafiti. Duniani hazipatikani kiasili tena hata kama uwezekano ya kwamba ziliwahi kupatikana zamani ila tu kutokana na maisha mafupi ya atomi zao zimeshapotea muda mrefu. Kama ingewezekana kuitengeneza kwa kiasi kikubwa kidogo inawezekana itakuwa na rangi kama [dhahabu] lakini hadi sasa atomi chache hazikutosha kutazama rangi.


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: