Nenda kwa yaliyomo

Berili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Berili
Jina la Elementi Berili
Alama Be
Namba atomia 4
Uzani atomia 9.01218
Valensi 2, 2
Ugumu (Mohs) 5.5
Kiwango cha kuyeyuka 1551 K (1278 °C)
Kiwango cha kuchemka 2750 K (2476 °C)
Asilimia za ganda la dunia 5 · 10−4 %

Berili ni elementi na metali ya udongo alkalini yenye namba atomia 4 na uzani atomia 9.01218 kwenye mfumo radidia. Alama yake ni Be. Jina linatokana na neno la Kigiriki βηρυλλος berillos linalotaja aina ya vito ambamo elementi hii iligunduliwa mara ya kwanza mwaka 1798 kama oksidi ya Berili.

Elementi tupu ina valensi mbili na rangi yake ni kijivu feleji. Ni metali ngumu sana na nyepesi. Katika kiwango sanifu cha joto na shindikizo berili haioksidishi kirahisi.

Kiasili inapatikana katika kampaundi mbalimbali. Aina zinazoonekana zaidi ni ndani ya mawe ya kito kama zumaridi.

Matumizi ya Berili ni hasa katika aloi za metali, hasa pamoja na alumini na shaba.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Berili kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.