Rutheni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Rutheni (Ruthenium)
Lulu ya gramu 1 ya Rutheni tupu
Lulu ya gramu 1 ya Rutheni tupu
Jina la Elementi Rutheni (Ruthenium)
Alama Ru
Namba atomia 44
Mfululizo safu Metali ya mpito
Uzani atomia 101.07
Valensi 2, 8, 18, 15, 1
Densiti 12.45
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 2607 K (2334 °C)
Kiwango cha kuchemka 4423 K (4150 °C)
Hali maada mango
Mengineyo haba sana

Rutheni ni elementi na metali haba sana duniani. Kikemia ni elementi ya mpito yenye kifupi cha Ru na namba atomia 44 katika mfumo radidia.

Tabia[hariri | hariri chanzo]

Hutokea katika mitapo ya platini au pamoja na madini mengine ya elementi za kundi ya 10 katika mfumo radidia. Rutheni ni metali ngumu na kechu yenye rangi nyeupe-kijivu inayopatikana kama fuwele.

Matumizi[hariri | hariri chanzo]

Matumizi yake ni katika aloi pamoja na platini, paladi, titani na wakati mwingine pia dhahabu kwa kusudi la kuongeza ugumu wa aloi hizi. Magusano ya umeme ya platini au paladi hudumu muda mrefu kama rutheni imeongezwa.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Jina la "ruthenium" linechaguliwa 1844 na mfumbuzi wa kwanza aliyekuwa Mjerumani Mrusi Karl Klaus kwa heshima ya Urusi kwa sababu "Ruthenia" ilikuwa jina la Kilatini kwa Urusi.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rutheni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.