Nihoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nihoni (Nihonium) ni elementi ya kikemia yenye alama Nh na namba atomia 113. Iliitwa pia eka-thallium. Haitokei kiasili maana ni elementi sintetiki inayoweza kutengenezwa katika maabara kutokana na mbunguo wa Moskovi.

Elementi hii ilitambuliwa mwaka 2004. Vikundi vya wanasayansi waliitafuta wakati uleule pale Dubna (Urusi) na Wako (Japani). Hatimaye Wajapani walikubaliwa kuwahi kutambua tabia zake nyingi wakachagua jina kufuatana na jina la kienyeji cha Japani, "Nihon". [1] , [2] , [3]

Nusumaisha ya Nihoni ni sekunde chache, kwa hiyo haikudumu muda wa kutosha kuangalia tabia zake; kila kiasi kinachotengenezwa kinapotea baada ya sekunde kadhaa. Hivyo hakuna matumizi kwa elementi hiyo yanayojulikana.

Kulingana na nafasi yake katika jedwali la elementi inawezekana ni metali laini yenye rangi ya fedha ikiwa na utendanaji mkali wa kikemia.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Morita et al., Experiment on the Synthesis of Element 113 in the Reaction 209Bi(70Zn, n)278113 Archived 5 Julai 2007 at the Wayback Machine., J. Phys. Archived 1 Julai 2007 at the Wayback Machine.
  2. press release in Japanese. Jalada kutoka ya awali juu ya 2007-03-01. Iliwekwa mnamo 2020-03-29.
  3. Japanese scientists create heaviest ever element

Tovuti za Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nihoni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.