Majadiliano:Virusi

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ngeli ya virusi[hariri chanzo]

Katika miaka iliyopita tulikuwa na majadiliano kuhusu ngeli ya kisarufi ya neno "virusi". Kufuatana na utaratibu wa kawaida "virusi" ni neno la kigeni lililopokelewa kutoka Kiingereza (au KIlatini cha kisayansi) ambako linataja umoja na uwingi pia. Lakini katika uzoefu wa wasemaji wengi wa Kiswahili neno hili limechukuliwa kuwa katika ngeli ya "ki-vi" hasa kwa sababu mara nyingi viini hivi hutokea kwa wingi na hivyo swali la kuvitaja kwa umoja halitokei mara nyingi. Baada ya kuomba ushauri wa TATAKI tutatumia neno hili kw kufuata ngeli ya ki-vi. Kipala (majadiliano) 07:02, 9 Novemba 2019 (UTC)[jibu]

Sawasawa, lakini tukifuata pendekezo lako, kiini kimoja kitaitwa kirusi? Siwezi kujizuia kucheka. ChriKo (majadiliano) 19:59, 10 Novemba 2019 (UTC)[jibu]

Kiswahili[hariri chanzo]

ni kali sana 196.207.162.154 18:56, 8 Mei 2023 (UTC)[jibu]