Shahawa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Picha ya shahawa wakati inajaribu kuingia ndani ya yai ya kike
Shahawa jinsi zinavyoonekana kwa hadubini

Shahawa (ing. sperm, spermatozoon) ni mbegu za mwanaume zinazozalishwa katika korodani. Kila shahawa ni seli inayoweza kutembea nje ya mwili.

Kazi yake ni kubeba kromosomu zenye habari za jenetiki (yaani tabia za mwili inakotoka) na kupitia kwenye uterasi ya kiumbe cha kike na kuingia ndani ya ovidakti ( mirija ya uzazi ya kike)huko ndani ya yai. Kuingia kwa shahawa ndani ya yai kunasababisha maungano ya DNA za yai na shahawa na ugawaji wa yai ambao ni chanzo cha kiumbe kipya.

Mfumo wa shahawa ni "kichwa" kidogo kinachobeba DNA na mkia mrefu ambao mwendo wake unasogeza shahawa mbele. Umbo hili linafanana na kiluwiluwi mdogo lakini ni seli 1 tu.

Shahawa ya kibinadamu huzalishwa katika korodani ya mwanaume. Kila seli ya shahawa ina kromosomu 23. Binadamu huwa na kromosomu 46 kwa hiyo shahawa inabeba nusu ya habari zinazohitajika kwa kuanzisha kiumbe kipya. Nusu nyingine inapatikana katika yai ya kike ambako shahawa inaelekea kuingia.

Wakati wa tendo la ngono shahawa inafyatuliwa nje ya mboo. Kama hii inatokea ndani ya kuma ya mwanamke shahawa inasambaa na kuenea ndani ya kuma. Ilhali idadi ya seli za shahawa ni kubwa sana ni seli zaidi ya millioni mia nne.( 400000000 seli) uwezekano ni mkubwa ya kwamba seli kadhaa za shahawa zinafika hadi ovidakti na kukuta yai iliyo tayari. Si zaidi ya seli 100 kati ya milioni zilizotoka ambazo zinafika kwenye yai. [1]

Yai iliyo tayari inapokea seli 1 ya shahawa tu. Hapa kromosomu 23 ndani ya yai zinaunganishwa na kromosomu 23 za shahawa na hapa kuna jumla ya 46 zinazotosha kuanzisha kiumbe kipya.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. SemenAnalysis Male Fertility Test, Sperm Count.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: